Utegi street!

Nimetumiwa picha hii  leo ikionyesha kibao cha mtaa wa kuingia nyumbani kwa mama yangu ikiwa na jina la kijiji alipozaliwa baba yangu ambacho kinaitwa UTEGI.

  Sina huwakika ni serikali za mitaa au wilaya / mkoa ndio unatoa majina ya mitaa ila mimi nimefurahi kwani huku Marekani  vitu kama hivi huwa ni big deal sana! Nimefurahije sasa 😍😍 kijiji chetu kinajulikana kimataifa ati! Simnajua kuna UTEGI International Ltd 🤣🤣🤣 Natamani ile bara bara inayokatiza toka NSSF kupitia kwetu watu wa Tanroad nao  wangeipa jina la “Otieno Igogo road” aaaah! Sasa hapo lazima nyumba yetu ingekuwa kati kati ya makutano ya Otieno Igogo road na Utegi  street itapendeza zaidi in Dr Shika’s voice 😍😍😍 (tazama picha hii 👇👇 kwa mfano tu)   kama nawaona wenye roho za kichawi! Watu wa Kansas city hakikisheni Robert Otto anaona hii picha maana anajifanya asomi hii blog 🙄🙄 mwambie soon Utegi inatinga USA  yani kama anaweza akimbie apande juu azibe au anywe sumu ya panya afie mbali!!! Na mtandao wote wa majungu najua mnasomaga hapa kama nawaona. Tatizo NYOTA AAA  🤣🤣🤣🤣🤣 nyota zenu zimefubaa hazingai 😂😂😂😂🙈🙈 anyway, hicho kilikuwa kibwagizo tu! Nimefurahi na namshukuru Mungu kwa yote!

2 thoughts on “Utegi street!”

Leave a Reply