Kutoka Facebook

FB_IMG_1441512219713Nimependa sana hii picha ya Mr and Mrs James Chanda. Wamependeza sana.

BTW,  James ni kaka ambaye tumefahamiana kwa miaka mingi sana. Tulikutana mara ya kwanza Buttler Community College, Andover, Kansas. Nikiwa nasubiria ride from my cousin brother China Igogo naye alikuwa anasubiri kuona adviser basi katika kuongea ndiyo tukajuana wote wa Tanzania na pia wanafahamiana sana na kaka yangu. Basi akampigia na kumwambia asije kunifuata yeye atanirudisha kwani ilikuwa inachukua kama saa moja hivi kutoka Wichita mpaka hapo college. Natoka hapo tukawa marafiki akawa siku ambazo anaenda shule huwa ananipitia na mimi kwa wakati huo nilikuwa sijajifunza kuendesha gari na ilikuwa msimu wa snow. James Asante sana. Uzidi kubarikiwa sana wewe na familia yako yote.

Leave a Reply