#TBS# Linda Bezuidenhout (LB)

11249848_709423412497306_3810608941086466482_nLeo nimeamua ku Throwback video za interview ambazo nilifanya na mwanamitindo wa kimataifa Ms. Linda Bezuidenhout mnamo mwezi wa pili mwaka huu 2015!

Hapo juu ? nisehemu ya kwanza ya mahojiano. Na hapa chini ? nisehemu ya pili au ya mwisho ya mahojiano yetu. Haya yalikuwa ni mahojiano yangu ya kwanza kabisa kufanya huku nikirekodiwa. Nilipewa hii nafasi ghafla, yani nilijua nataka kufanya mahojiano na Linda lakini sikujua lini yatafanyika. Mara ilikuwa siku ya juma Tatu napigiwa simu na kaka yangu Dj Luke wa Vijimambo blog nakuambiwa kuwa Linda ametukaribisha kwake siku ya Juma Mosi na yupo teyari kufanya mahojiano nami! Nilisita, lakini kaka yangu akasema nitaweza nisiogope! Basi hivyo ndivyo ilivyokuwa. Kama hujawahi yaona basi nakuomba uyatazame na niruhusa kutoa maoni yako!

Wiki hii inayo anza kesho, Mungu akijalia nitaelezea mambo fulani kuhusu Linda, na nini msimamo wangu mimi kama Alpha Igogo kuhusu mambo au maugomvi ambayo Linda anahusika nayo kwenye mitandao. Najua kuna baadhi yenu mnataka kujua mimi nasimama wapi kwani mlishawahi kuniuliza. Basi tuombeane uzima. Mbarikiwe wote!

Leave a Reply