Walijua hili?

Okay, wanawake wenzangu ambao mnapenda kuvaa lace wigs.  Siunajua lazima ukate ile lace pale mbele na sanyingine lace huwa inabaki kidogo, na mara nyingi huwa inaoneka kwasababu huwa haifanani na ngozi ya kichwa chako. Naomba uzingatia yakwamba; hii ni kwa zile 100% lace-wigs na siyo other types!

lace-wigBasi nimejifunza (from The Real Talk Show) kuwa unaweza uka chukua maji ya moto na majani ya chai (black), tengeneza chai weka majani mengi halafu chukua lace-wig yako  dumbukiza kwenye chai. Siyo yote, ni ile sehemu yenye lace tuu. Acha ikae kama kwa dakika 20 hivi au zaidi inategemea na how dark you want. Inabidi uishikilie ili isidumbukie yote au kama unakiti kinaweza kuishikilia napo sawa.

Leave a Reply