“Usimwangushe”-Dina Marios

USIMWANGUSHE ……..Kama ungependa kukumbushwa basi napenda ni kukumbushe,kuna mtu anakufikiria mno,kuna mtu ana ringa kwa ajili yako,kuna mtu mahali ana kujali sana hujajua tu,kuna mtu anakukumbuka sana,kuna mtu anatamani kuongea na wewe,kuna mtu anatamani angalau ashike mkono wako tu,kuna mtu anafurahia sana kukufahamu,kunamtu anashangilia kila hatua njema unayoichukua.

kama unapenda kuendelea kukumbushwa zaidi kuna  mtu anatamani kukupa zawadi na anakuona wewe ni zawadi kutoka kwa Mungu. Kuna mtu anakuelewa sana,kuna mtu anakupenda sana,kuna mtu anatamani japo acheke na wewe kidogo,kunamtu anakuombea mafanikio na kuna mtu anatamani japo ashike bega lako.

Songa mbele maana mafanikio yako ni ya huyu mtu pia ….. Usisahau kila mtu hata wewe unavaa kitambuliso kimeandikwa “natamani kutambuliwa na kuthaminiwa”  USIMWANGUSHE BASI!!! FB_IMG_1457053732155-1Nimependa sana blouse ya Dina. So nice na imempendeza sana. 

Leave a Reply