Birthday wishes

FB_IMG_1441031960530Kheri ya siku ya kuzaliwa kaka yangu kipenzi Noah Manongi! Niseme nini mimi Alpha?! Baba wa Mbinguni anajua yote yaliyopo ndani wa moyo wangu jinsi ninavyo kushukushuru kwa uwepo wako katika maisha yangu huku nilipo mbali na familia yangu! Umekuwa Nami kaka yangu katika tabu na raha, umekuwa nami hata pale ambapo mimi  mwenyewe nilikuwa sina imani nawe. Umesimama nami bila kutetereka hata pale baadhi ya marafiki zako walipo geuka na kunijengea chuki ambazo hazielezeki! Kaka yangu wewe hukuniacha kwani wanijua mimi jinsi nilivyo  na hukuogopa wala kuona haya kusimamia ukweli! Niseme nini kaka yangu? Kwakweli sina cha kusema zaidi ya Asante! FB_IMG_1441031782827Katika siku hii ya leo, siku ya kuzaliwa kwako kaka yangu, namwomba Mwenyezi Mungu mwenye wingi wa rehema azidi kukulinda, siyo akubariki bali azidi kukubariki kwani wewe teyari ulisha barikiwa! Mungu akupe afya bora, amani, furaha, na upendo ndani yako na ndani ya familia yako. Hekima yako na upendo  wako vikapate kuongezeka maradufu! Ukaguse na kubariki maisha ya watu wengine kama ulivyo fanya kwangu mimi. Happy birthday my brother. Love you deep!

4 thoughts on “Birthday wishes”

Leave a Reply