Category Archives: politics

“It is morally wrong to punish them for their efforts to better themselves; regardless of how they seek to better their lives”-Chege Kilahala

Nakumbuka enzi za Nyerere……wakati alipokuwa anakamata vijana wasio na kazi kwa kosa la “uzururaji”…..kwangu mimi naona kazi ya serikali ni kuweka sera za kuinua uchumi na kuongeza kazi (to create economic policies that will create opportunities for young people)…….kukamata vijana ambao wanatafuta riziki wakati serikali yako imeshindwa kuinua maisha yao kwa kuweka uchumi bora ni “morally wrong”. Na nalaumu hiyo sera ya Nyerere wakati ule. Nyerere was supposed to own his failure; failure to enact laws that will create policies for economic opportunities for young people.

Likewise, while I don’t support impersonation and forgery, I think we should be considerate of people who seeks second chances in life…..using other people’s certificates to advance their career opportunities etc etc

Who is to blame for that? Again; the government and its education policies. For not enacting laws that will give second chances to these kind of people. In most developed countries, you can opt for other educational alternatives that are equivalent to the education level you seek.

The govt needs to work harder to create an environment in which people who failed in their exams, young girls who caught pregnancies while at school and other who dropped out of school for any reason, can do “a comeback” later in life. Lack of opportunities and alternatives makes these people turn to forgery and impersonation.

It is “morally wrong” to punish them for their efforts to better themselves; regardless of how they seek to better their lives (except if its killing or stealing).

TATIZO MMEKUBALI KUCHEZA NGOMA ZINAZO PIGWA NA UPINZANI.- Peter Sarungi

 Kwenye ngoma zetu kuna wanao piga ngoma na kuna kundi la wanao cheza ngoma inayopigwa. Siku zote mpiga ngoma ndiye mwamuzi wa aina gani ya mdundo upigwe ili mcheza ngoma acheze, mpiga ngoma akizima ngoma basi na mchezaji naye anasitisha kucheza, mpiga ngoma ndiye ana amua speed ya ngoma ama ngoma ipigwe kwa muda gani.

Siasa za sasa za nchi ziko kisayansi sana kiasi kwamba upinzani wametawala njia nyingi za upashaji habari. Siasa hii naifananisha na ngoma zetu za jadi, yaani ni kama vile upinzani wanapiga ngoma ili watawala wacheze.

Hii ngoma ya wapinzani imeanzwa kuchezwa tangu mwaka jana baada ya utawala mpya kuanza kazi, upinzani umeshapiga ngoma kwa midundo mingi sana tofauti iliyomfanya mtawala kucheza bila kuchoka.

Hizi ni baadhi ya ngoma zilizopigwa na upinzani na watawala wakacheza kwa maana ya kujibu mapigo.

1. Ukuta

2. Uchwara

3. Phd

4. Michango ya Tetemeko

5. Njaaa

6. Bring back ben alive

7. Free Lema

8. Free Max wa JF

9. Swala la uteuzi wa wabunge

10. Bashite

Haya ni machache yaliyo vuma na kuchukua headlines za magazeti na mitandao ya jamii. Na hizi zote zimekuwa zikianzishwa kwa malengo ya kuonesha na kuaminisha mapungufu ya serikali kwa wananchi.

Siwalaumu upinzani maana hiyo ndiyo sayansi ya siasa na ndiyo kazi yao, ila nawalaumu sana chama tawala na watawala wenyewe kwa kushindwa kupiga ngoma zao ili upinzani nao wacheze. Ninavyojua mimi, JPM amefanya mambo makubwa ambayo yanatosha kuwekwa kwenye haedline kwa muda mrefu, lakini wasaidizi wa watawala na wapenzi wa chama tawala wamekaa kimya na kujikuta wakijibu mashambulizi ya upinzani katika hoja zao bila kujua kwamba wanacheza ngoma. Hizi kick ndizo zinazo pamba upinzani usisahaulike hadi 2020 hata kama mkikataza siasa za majukwaa.

Au labda watawala wamejitoa kwenye ulingo wa siasa? Au wapenzi wa chama tawala wameshindwa kuusoma mchezo wa siasa? Huu mchezo hautaki hasira wa mabavu ya dola ila unataka mkakati wa kujivunia mazuri yanayo fanywa na Utawala Chama tawala kukaa kimya na kucheza ngoma za upinzani ni sawa na huyu ☝ aliye kabidhiwa brifkes ya ofisini akaringa bila kujua kuwa imetoboka. Amkeni mpige ngoma wapinzani wacheze, fanyeni kama Magoiga SN.

Asanteni

First Lady by default! Sasa ni Mbunge wa kuteuliwa!

Malkia wetu wa nguvu anarudi tena kwenye macho ya jamii! Mama Salma Kikwete anarudi tena baada ya kuteuliwa na Rais Dr. Magufuli kuwa Mbunge wa bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania hapo jana!

Wengi tulimzoea kumuona akitumikia jamii kama First Lady lakini sasa atatumikia jamii kama Mbunge. Ile nafasi ya kwanza ya kuwa First Lady ilitokea tu (by default) kwasababu ni mke wa JK. Lakini sasa lazima atakuwa ameombwa na Rais Magufuli na amekubali kwa hiyari yake mwenyewe! Hata hivyo, nani ajuae?! yawezekana hata akapewa wizara fulani kuiongoza ambapo binafsi naamini atafanya kazi nzuri sana kwani ametuonyesha kwa vitendo alivyo kuwa First Lady! Haswa natamani apewe wizara inayo husiana na mambo ya maendeleo ya wamama na watoto!

Katika maisha kila mtu ana ndoto zake na wito wake. Watu wengine wamebahatika kuweza kutimiza ndoto zao wakiwa na umri mdogo. Lakini kuna wengine kwasababu ambazo pengine ni Mungu tu ndio ajuae ndoto zao huchelewa kutimia na wengine zisitimie kabisa! Basi si ajabu kumuona Malkia wetu wa shoka akitumikia jamii tena akiwa na cheo cha chini. Kwani hiyo ni dalili nzuri ya mtu mnyenyekevu ambaye yupo teyari kujishusha kwa faida ya taifa lake. Pia bado haja chelewa kutimiza ndoto zake ndio maana hata Hilary Clinton alikubali kufanya kazi ya kuwa Secretary of State chini ya uongozi wa Rais Baraka Obama.

Hivyo basi, tunamtakia utumishi mwema kwa kuweka uzalendo kwanza. Natumaini ile kauli mbiu yake ya “Mtoto wa mwenzio ni wako” ataiendeleza ili kuokoa vijana wa taifa hili kutoka kwenye madawa ya kulevya!

**Huko nyuma niliwahi sema hivi juu ya mama Salma Kikwete,  “Kwaheri ya kuonana mama Salma Kikwete ” **

Kulipwa kwa kazi ya campaign ya chama ni halali yako!- Alpha Igogo

Alpha Igogo
Blogger

Katika kila jambo au shughuli yoyote lazima kuna fedha zitatumika tu! Hii haijalishi ni shughuli ya chama, kanisa, msikiti, kijamii, au za kipagani lazima fedha zitahusika! Lakini sasa uingizaji na utoaji wa hizo fedha zinaweza kuwa katika mfumo uliyo rasmi (yani kuna kuwa na budget, mfumo wa malipo, na washuhudiaji) au siyo rasmi (yani hakuna accountability ya aina yoyote ile).

Tukirudi katika mada yetu kama kichwa cha habari kisemavyo, kuwa, “kulipwa kwa kazi ya campaign ya chama ni halali yako” basi ngoja tuzungumzie hilo kwa sasa. Kampeni za siasa huwa lazima chama kinajipanga kwa mikakati (strategies) ya jinsi ya kufanya campaign yenye mafanikio. Na moja ya mikakati hiyo ni jinsi ya kukusanya pesa rasmi kwaajili ya kukamilisha mikakati hiyo! Hapo ndipo utasikia kitu ‘budget ya campaign’. Pia kwa serikali ya Tanzania huwa wanakitu kinaitwa posho / ruzuku ya chama wakati wa campaign!

Hiyo budget ya campaign haitumiki tu kununulia vitendea kazi vya campaign bali pia kuwalipa wanachama / makada watakao kuwa teyari kufanya campaign hiyo kulingana na malengo ya chama chao. Ndio maana wakati wa campaign huwa wana aajiriwa watu maalum wa kufanya campaign au kikosi maalum cha nguvu kazi kwa ajili ya campaign husika kwa mfano anaweza ajiriwa Campaign Manager, au Financial Controler kwa ajili hiyo tu!

Sasa wewe kama ni mwanachama uwe mtu wa kawaida au “celebrity” kupewa fedha kwa ajili ya campaign ni kitu cha kawaida, ni swala ambalo linatambulika kisheria, na zaidi ya yote ni halali yako!

Wewe unapo acha shughuli zako za uzalishaji wa kila siku nakwenda kufanyia chama campaign nilazima chama kikupe hela za kujikimu maana utahitaji hela ya kukutoa point A to Z, utahitaji kula, utahitaji kulala kama ni nje ya mahala unapo ishi! Huwezi kuchukua pesa zako binafsi kufanyia chama campaign wakati kwanza umeacha shughuli zako za uzalishaji, pili kama una familia inamaana budget ya familia utaivuruga kwa mambo ya campaign.

Jamani, hata makanisani kuna budget ya kutembelea washiriki ambao ni wagonjwa, wajane n.k nawatu huwa wanapewa pesa za kujikimu na safari kama hizo. Hivyo si ajabu mtu kulipwa kwa shughuli ya campaign kwani hizo ndizo zile hela wenyeviti na viongozi wengine wa chama wanatumia kwa matumizi yao binafsi haswa kama hakuna mwanachama au wanachama ambao wanaweza ku-question uongozi! Kiwango / kiasi cha ulipwaji waweza tofautiana kutokana na nguvu aliyo nayo mtu huyo pamoja na makubaliano yao. Fedha zote zinazo ingia kwenye budget ya campaign ya chama lazima ziwe kwenye mfumo rasmi unao eleweka! 

Labda kama baba yako ni Mzee wa “Vijisenti” (you don’t need that kind of “petty” money)  kama sivyo kulipwa kwa kazi ya campaign ya chama ni halali yako!

Mungu ibariki Africa. Mungu ibariki Tanzania.

 

 

HATA SAULI ALIKUJA KUITWA PAUL! -Peter Sarungi

HATA SAULI ALIKUJA KUITWA PAUL Injili ya Yesu kristu inaeleza kuwepo kwa Sauli aliyebadilika na kuitwa Paulo. Injili inamwelezea Sauli kama kiongozi wa kijeshi aliyekuwa ni katili kupita kiasi, asiyekuwa na huruma, aliye chukia, kuwatesa na kuwa hukumu kifo wana wa Mungu. Lakini pamoja na machukizo haya yote mbele za Mungu bado Mungu alikuwa na mpango mzuri naye.

Mpango wa Mungu ulikuja kutimia na Sauli akaitwa Paulo. Kupitia jina la Paulo, tabia zake zilibadilika na akawa mtumishi wa Mungu aliyeweza kuhubiri injili na kuandika vitabu vingi vya injili kuliko wanafunzi wote wa Yesu kristu alio wachagua na kuwapa kazi ya kueneza injili. 

Hivyo sishangai kama Daudi akikimbia jina lake na kuitwa Poulo, maana yawezekana kwa jina la Daudi alikuwa mnyonge, kilaza, mvivu, mwoga, aliyefeli kwa kupata fa fa fa zote katika matokeo ya fom 4. Lakini kwa kuitwa Paulo emebadilika na kuwa jasiri, mchapa kazi, kiongozi mbunifu na mwenye kuthubutu, aliye faulu hadi chuo kikuu, aliyetenda makubwa katika uongozi wake kuliko hao wateule wa Mkuu. 

#MyTake 

Na Peter Sarungi (The next Speaker)

Kuna majina mengine yana Nuksi, hayaendani na ndoto zako na wala hayakusaidiiii. Unaweza ukawa una lalamika kushindwa kila jambo jema unalo jaribu kwa nguvu zote huku ukimshirikisha Mungu wako bila mafanikio kumbe ume sahahu kwamba jina lako halijabeba future unayotaka. Tuchunguze majina yetu hasa haya ya Ulaya.

Mwanangu Fidele siku akiona jina lake halimsaidii kufikia ndoto zake nitamruhusu na kumsaidia kubadili jina ???? Joks..

Lemutuz:- Mjadala wa vyeti hauna tija!

UKIWA MDHAMBI USIHUKUMU WADHAMBI- Peter Sarungi

UKIWA MDHAMBI USIHUKUMU WADHAMBI. 

Na Peter Sarungi (The next Speaker)

Niliwahi kusema kwamba vita alivyo chagua Makonda ni vita vinavyo hatarisha ustawi wa maisha yake. Mpaka sasa Mh. Makonda anapigana vita nne kwa yeye kuanzisha vita moja ya madawa.

1. Vita juu ya uhalali wa mali zake

2. Vita juu ya uhalali wa Elimu yake

3. Vita vya kisheria dhidi yake mahakamani

4. Vita dhidi ya Bunge na maazimio yake Maandiko matakatifu yanaeleza jinsi Yesu kristu alivyotoa kauli kwa wayahudi waliotaka kumwadhibu mwanamke aliye fumaniwa akizini kwa kutumia sheria za Musa……Alisema, “Kama kuna aliye msafi(asiye na dhambi) kati yenu basi na awe wa kwanza kumpiga mawe huyu mwanamke aliyefanya dhambi”

Hii ni kauli nzito sana kwa dunia ya sasa, Dunia inayotawaliwa na uwazi na kumbukumbu za kiteknologia, Dunia iliyo na macho pande zote, Dunia iliyojaa unafiki, usaliti, chuki, visasi, uongo, uzandiki, kashfa, fitina na machikizo mengi baina ya binadamu mmoja na mwingine.

Kwa Dunia kama hii… Ni vizuri tukaishi vizuri na jamii, tukaheshimu uongozi kam dhamana, tukajitakasa na dhambi kabla ya kuwatafuta na kuwahukumu wenye dhambi, tukajifunza kubakisha maneno ya kesho na keshokutwa.

Pole Mh. Makonda, ulianzisha vita moja lakini sasa unapigana vita nne tofauti.

Mungu akusaidie na akulindie roho yako isije ikapondeka kwa maneno na matendo ya binadamu wenzio…..Amina

2020 ni Pagumu!- Peter Sarungi

                    2020 NI PAGUMU!

Na Peter Sarungi (Next Speaker)

 Ikatokea Mungu akakubariki kufika 2020 ukiwa hai na mwenye afya nzuri basi utakumbana na changamoto ya joto kali la siasa ambalo halijawahi kutokea nchini. Kwa Lowasa Edward, 2020 ni mwaka wake wa mwisho kujaribu kufikia ndoto zake za kutawala nchi, ni kama ana bunduki iliyobaki na risasi moja ndani ya mapambano, hivyo ni lazima apambane kwa akili sana tena kimya kimya ili kutafuta target sahihi ya kufyatua risasi yake kwa adui. Ndio maana kwa sasa Lowassa anajipanga kimya kimya akiamini matokeo yake ni 2020.Kwa JPM, 2020 ni mwaka wake wa kuimarisha utawala wake na hasa kupata matokeo yatakayo leta taswira ya kupwaya kwa upinzani nchini. Hivyo kwa sasa anajipanga kwa matendo na kwa mifumo ndani ya chama na nje. Kutokana na nguvu alizopewa Raisi kupitia katiba ya nchi, ni kazi nyepesi sana kutengeneza mfumo utakao kusapoti mbele ya safari hivyo tutegemee mifumo hiyo kukamilika 2019.  

Kwa wananchi, 2020 ni mwaka wa majaribu sana kwao. Mpaka sasa bado wananchi wengi hawajui mwisho wa utawala huu ukoje, hawajui kama kutakuwa na mazuri ama mabaya ndani ya miaka hii mitatu iliyobaki (2017, 2018 na 2019) ikitokea uchumi wa mwananchi ukakua hadi kufika kipindi cha JK basi JPM atakuwa amepiga risasi ya ushindi kwa wananchi maana mpaka sasa amefaulu sehemu kubwa hasa ya ufisadi na nidhamu lakini amefeli kwenye UKATA wa wananchi, kuna malaika wameanza kuishi kama mashetani. 

Kuna Hash tag mbili zinazovuma mitandaoni

1# Nitamchagua tena 2020

2# Usirudie kosa 2020

 

Tafakari…. Chukua Hatua.

ASANTE JPM KUBARIKI VITA HII (Sehemu ya II)- Peter Sarungi

 

Na Peter Sarungi (Next Speaker)“Vita ya dawa za kulevya haina umaarufu, haijalishi ni mtoto wa nani anahusika, hata kama ni mke wangu anahusika mkamateni” Raisi Dkt. Magufuli…….Katika vita hii, nilikuwa nasubiri kauli ya mkuu wa kaya ya kutoa support ya ulinzi, usalama na hata kubariki vita hivi alivyo vianzisha Mh. Makonda (RC. Dar)  Kauli alizozitoa Mkuu wa kaya wakati wa kumwapisha Mkuu wa Majeshi Tanzania yana ashiria ushiriki wa moja kwa moja wa mkuu wa kaya. Majibu ya JPM kwa kauli ya Mh. Nape ni firimbi kwa viongozi wengine wanao leta sababu nyingi za kunyamazisha vita hii wakati vijana wana angamia. 

“Kauli ya Raisi ni agizo linalo hutaji utekelezaji bila kusita” Peter Sarungi @2017

TUSIBEZE VITA HII (Sehemu ya I)- Peter Sarungi

 Tusibeze uthubutu wa mtu tena kijana wa kawaida ambaye bado hajawa nguli katika siasa wala uongozi. Tumpe muda maana hiyo vita aliyoichagua ni vita ngumu inayo hatarisha maisha yake. Huyu ndiye kiongozi pekee wa kumuombea tofauti na wengine. Huyu yupo kwenye vita ambavyo kama wewe ungepewa fursa ya kuwa mkuu wa mkoa huu basi inawezekana ungeshindwa kudeal hata na dagaa kama Makonda alivyoanza. Tumpe moyo mkuu na kumwombea kwa Mungu apigane vita vizuri, naamini hata kama hatashindwa kufikia mafanikio tunayoyataka lakini atakuwa amefanya sehemu flani ya kutatua uovu huu ambapo mwingine atakaye jitokeza katika vita hiyo ataanza alipo ishia Makonda. Hatuwezi kunyamaza kimya kwa tatizo kubwa kama hili na asitokee hata mtu mmoja wa kusema hata kidogo alafu tukajiona tupo samala, Laa hasha kukaa kimya ni kuhalalisha uwepo wa tatizo. Vijana wengi wana angamia na kupoteza nguvu kazi na vipaji kwa sababu ya kukaa kimya na hata kubeza jitiada hizi ndogo zinazo chukuliwa na Makonda. Tuungane na Makonda kutenda na kufikiri tofauti kwa kuchukua hatua za kutenda badala ya malalamiko na matamko yasiyo isha wala kusaidia jamii. Tuweke siasa pembeni kwenye majanga makubwa kama haya ili kuunga kila hatua zitakazo chukuliwa na yeyote katikakupambana na Tatizo hili. 

Na Peter Sarungi (Next Speaker)

Asanteni..

Sabato Njema wana wa Mungu.

WIZARA INA MIKAKATI GANI JUU YA WATU WENYE WALEMAVU TANZANIA?- Peter Sarungi

Na Peter Sarungi (Next Speaker)

Watu wenye ulemavu ni moja ya jamii iliyo katika makundi nyonge (kwa sasa tumefika milioni 4 kwa idadi). Makundi mengine ni kama wazee, watoto na wanawake, makundi haya yanaitwa ni makundi nyonge kwa sababu yana mahitaji maalumu ya kibinadamu na hayawezi kumudu ushindani ulio sawa katika jamii hivyo ni lazima jamii pamoja na serikali iyatizame kwa jicho la tatu lenye utu, huruma na upendo ili nao wajione wapo katika nchi yao na waweze kuonesha uwezo wao ambao Mungu amewakirimu pasipo kujali mapungufu waliyo nayo. 

Peter Sarungi akiwa na dada zake; Alpha Igogo (kushoto) na Magreth Igogo (kulia) nyumbani kwa Peter huko Chanika.

Mimi ni Mlemavu lakini hata wewe ni Mlemavu mtarajiwa maana kama bado unaishi duniani basi jua Mungu bado anaendeleza uumbaji wake kwako. Hivyo linapotokea jambo linalohusu ulemavu basi jihisi na wewe ni mhusika kwa namna moja ama nyingine.

Katika uchaguzi uliopita 2015, nilitoa tamko kupitia jumuiya za watu wenye ulemavu Tanzania ambao ulilenga kueleza changamoto za walemavu pamoja na mapendekezo yake. Changamto kuu nilizoziainisha kwa msisitizo ni ushirikishwaji wa watu wenye ulemavu katika vyombo vya maamuzi pamoja na muundo wa kusimamia maswala ya watu wenye ulemavu. Niliamini kuwa ili kutibu changamoto hizi za elimu, ajira, afya, uchumi, siasa na huduma zingine ni vizuri tukashirikishwa katika kupika chakula na kukiandaa mezani.

Nilifarijika sana baada ya Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutangaza baraza la Mawaziri pamoja na muundo wa wizara zake, kwa kweli mhe. JPM alitutendea haki ambayo haikuwahi kutendwa na tawala tangu kupatikana kwa uhuru wa nchi. JPM alisikia kilio cha watu wenye ulemavu kwa kutenga wizara itakayo husika na maswala ya walemavu tena ikiwa chini ya ofisi ya waziri mkuu kama tulivyotoa kwenye tamko na pia akateua waziri mwenye asili ya ulemavu (dr. Abdallah posy) na makatibu wa wizara wawili wenye ulemavu akiwemo mwanasiasa Amon Mpanju ili kushiriki kupika chakula cha walemavu. Hakika baada ya uteuzi huu, jamii ya qatu wenye walemavu tulianza kuona nuru na kuona matumaini ya kula chakula tulichoshiriki kukipika na kukiandaa mezani. Nampongeza sana Raisi kwa moyo huu wa kujali makundi manyonge katika jamii(Mungu azidi kumpa afya tele na azidi kutetea wanyonge kama anavyofanya sasa)

TATIZO NI NINI?????

Kwa mtazamo wangu, bado naona hakuna mabadiliko chanya yanayoletwa na wizara hii hasa kutoka kwa waziri husika Mh.Posy. Bado mifumo ya unyonyaji imeendelea kuwepo kwenye vyama vya watu wenye ulemavu, bado uchumi umezidi kudorora kwa watu wenye ulemavu, bado Elimu imekua duni na garama kwa watu wenye ulemavu, Bado siasa haiwatambui watu wenye ulemavu kwa vitendo, Bado sheria No 10 ya watu wenye ulemavu imewekwa kando, Bado ajiri imekuwa ngumu na ya kubagua watu wenye ulemavu na bado huduma bora imekuwa ni kitendawili kwa watu wenye ulemavu.

Je ni nani wa kututetea? Ni nani wa kutusemea kama sio Mh. Posy na wenzake akina stella ikupa, Dr. Macha, Amina Mollel, Amon Mpanju na wengine walio katika kundi hili?. Ni nani wa kulaumiwa ikiwa JPM ametupa nafasi kupitia hawa wenzetu alafu wamekaa kimya? Ni nani wa kuonesha mfano na kuaminisha jamii juu ya uwezo wetu kama sio akina Posy, Mpanju, macha, stella na wenzake? Ni nani wa kupiga kelele juu ya mateso na manyanyaso wanayoyapata wafanyabiashara walemavu wa Tanzania kama sio akina Mh. Posy, Mpanju na wenzake waliopata fursa? Ni nani wa kutuunganisha watu wenye ulemavu na kupata fursa za uchumi na siasa kama sio hawa walio teuliwa na JPM? Mbona wamejisahau utafikiri hawajatoka katika kundi hili? Au wanadhani fursa waliyopata ni kwaajili yao peke yao? Au ndo kusema ni aibu na dhihaka kuwa mlemavu na kutetea jamiiyako? Mbona kasi ya JPM inawaacha mbali? Tatizo ni nini?

Tulikaa kimya na kuwapa ushirikiano ili kuona matunda ya kushirikishwa katika kupika chakula lakini inakaribia mwaka sasa hatuoni kama chakula mnachotupikia ni kizuri…

Tafakarini na chukueni Hatua…. 

Tafadhali, naomba ifahamike yakuwa hii article iliandikwa wiki mbili zilizopita wakati Dr. Posy akiwa bado ni Waziri. Lakini sasa nafasi yake ipo wazi!

“Sometimes I really wonder!”- Sandra Mushi

Sometimes I really wonder! How we can just wake up and pull ‘sherias’ out of our hats. Sasa ati no spot lights, no fog lights and no tints …

How about you install street lights on ALL streets and actually have them ON and working; and how about having proper and working security measures including when I come report a theft, you actually attend to it and FOLLOW it up!  Instead of asking for ‘chai’ na ‘nauli’ kila kukichwa.

Those lights are our safety so I don’t have to worry about driving into a bridge on a dark night.  They are my safety so I can see clearly on a rainy day.  They are my safety so I can see that drunkard staggering from a far even before I get to that corner.

Those tints are our safety so I don’t have my windows broken as I am sitting in a meeting simply because the street boy saw my gym bag on the back seat.  They are my safety so when they want to follow me home they are not sure who is in the car.  They are my safety so that conniving motor cyclist does not see that its a lone woman driving.

Hembu do your due diligence basi and assure us of our safety before you mercilessly start imposing this ‘out of the hat’ sheria on us.

You do your part and we will humbly oblige and do ours.

Wametugusa sana; watakumbukwa daima!

Rais Obama anaweza asiwe the best President in American history. Lakini ni ukweli usio pingika kuwa they were the best 1st family ever!!……..Wamegusa miyoyo yetu, wamebadilisha mitizamo ya familia nyingi kwa kuonyesha jinsi gani family should look like! Mr and Mrs Obama wameonyesha mfano bora wa jinsi gani couple  should respect and support each other for the goodness of the family and your country! Wamekuwa mfano mwema wa wazazi jinsi ya kulea humble children pamoja na kuwa na access to everything they wanted! Wamegusa nafsi za watu wengi sana na kuacha their own legacy kwenye hii dunia! Tutawakumbuka siku zote, Mungu azidi wabariki!

Rwanda has started legislative process to Make Swahili one of the official languages!

Hon. ShyRose Bhanji

Presenting the Motion to congratulate Rwanda for Starting a legislative process to make Kiswahili one of the official languages in Rwanda. This is highly commendable move and should be strongly supported by all stakeholders who have EAC integration at heart. #Kiswahili #OnePeopleOneDestiny …. #Nikiwasilisha Hoja bungeni ya kuipongeza Rwanda kwa Kuanza mchakato wa kutunga sheria ya kukifanya Kiswahili kuwa moja ya lugha rasmi nchini Rwanda. Hatua hii inahitaji kuungwa mkono na wadau wote ambao ni waumini wa mtangamano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki. #UmojaWetuNiNguzoYetu

#EalaInKampala

HUYU ANA MOYO MKUU…..by Peter Sarungi

Na Peter Sarungi (Next Speaker)Kwa sasa ni nadra sana kupata binadamu walio umbwa na Moyo Mkuu, moyo unao weza kuhimili shida, kejeli, dharau, matusi ma vikwazo mbalimbali vyenye lengo la kulainisha Moyo. Mh. Lowasa Edward alikumbwa na kashfa akiwa CCM tena Waziri Mkuu, akasemwa na kutukanwa na viongozi, wanachama na wapenzi wa chama kikuu cha upinzani Chadema Tanzania, huku akiitwa Fisadi nchi nzima… Alikaa kimya bila kujibu.

Alipo hama CCM kwenda CDM, CCM walimuona kama msaliti ingawa kwa CDM alibadilika na kuwa Malaika. Bado aliendelea kutukanwa, kudharauliwa na hata kuombewa mabaya na viongozi, wanachama na wapenzi wa chama tawala kipindi cha uchaguzi 2015… Alikaa kimya bila kujibu.

Pamoja na yote hayo, bado ameendelea kuwa na Moyo Mkuu kwa nchi yake. Huyu namfananisha na Mh. Raila Odinga wa Kenya na Mh. Kiiza Besige wa Uganda kutokana vikwazo wanavyopitia. Mungu awatimizie haja ya mioyo yao.

Tujifunze kitu hapo, unajifunza nini?

MH. LOWASSA ANAIJUA SIASA YA TANZANIA-Peter Sarungi

Peter Sarungi a.k.a Next Speaker a.k.a Baba Pilato

Siasa za Tanzania bado hazieleweki kwa wananchi wengi na mimi nikiwemo. Wengine wanaiita siasa maji taka, siasa za kujipendekeza, siasa za mafigisu, siasa za mamluki na usaliti, siasa za propaganda, siasa za nguvu ya umma na nguvu ya dola, siasa za uongo, siasa za kidiplomasia, siasa za matukio, siasa za maigizo, siasa za maonyesho na mimi kwa sasa naziita siasa za Mwendo Kasi.Kwa Tanzania, ni Mh. Lowasa Edward pekee anaye jua siasa za nchi, anayeweza kubadili njano kuwa nyekundu, anayeweza kupanga na kupangua, anayeweza kubadilika kutokana na mazingira, anayeweza kumpenda adui yake hata kwa unafiki, anayeweza kubadili msimamo wa mpinzani wake, anayeweza kumbadili mpinzani kuwa mfuasi wake, anayeweza kupiga ngoma kisha serikali ikacheza, anayeweza kuwa na chama ndani ya chama, anayeweza kusababisha mafuriko ama hata kuyatengeneza, anayeweza kusababisha taharuki mtaani anapo onekana nahata kuwapa hofu watawala.

Kumekuwepo na kauli nyingi za kukubali ama kukataa uwepo wa njaa na uhaba wa chakula kwa muda wa zaidi ya wiki bila kuwepo kwa solution. Lakini Mh. Lowassa alipokuja na kauli ya kuwa na nia ya kutafuta chakula kwa ajili ya wahanga kwa madai kuwa Mkuu kakataa kutoa chakula kwa wahanga ikiwa ni sehemu ya kuleta suluisho la tatizo, jana serikali ikajibu mapigo kwa kusema ita sambaza chakula na ina hifadhi tosha ya chakula.

Viongozi kama akina Mh. Lowassa ni muhimu sana kwa jamii yetu hata kama wasipo weza kutawala nchi lakini uwepo wao na uwezo wao katika siasa za nchi intosha kufanya mabadiliko nje ya ya mfumo rasmi na kuleta matokeo chanya ya maendeleo..

Tutafakari kwa matendo bila hisia za vyama.

MATOKEO YA KELELE ZA #BringBackBenAlive NI YAPI NA YAMEISHIA WAPI?- Peter Sarungi

Peter Sarungi a.k.a The Next Speaker-Baba Pilato!

Watu wa Makabila yanayo patikana mkoa wa Mara (Kwetu Pazuri) wana desturi ya kuwa jasiri, wakweli na wenye uwezo wa kusimamia jambo analo liamini. Lakini huku jijini Dar tulipokuja kutafuta maisha, mambo yake yanaendeshwa kwa usanii, unafiki, uoga, dilli, uongo na kutafuta kicky pasipo sababu ya msingi.

Uozo huu umeingia hadi kwenye siasa kiasi kwamba huwezi kutofautisha siasa za chama tawala na zile za Upinzani yaani wote wamekuwa wafuasi wa mambo hayo ya jijini.

Wahusika Tuelezeni, kwanini mpo kimya kwa swala mlilo lianzisha? na mtuambie matokeo chanya ya #Bring_Back_Ben_Alive ?

Msianzishe kampeni katika mitandao halafu mkaziacha katikati bila kujua hatima yake, What if Ben amedhurika? Kelele zenu na ukimya wa Ghafla utakuwa umemsaidia nini Ben? Tafakari, Chukua hatua… 

SIASA NA DEMOKRASIA YA KENYA….. TUNAJIFUNZA NINI KATIKA MIFUMO YAO??-Peter Sarungi

 

Peter Sarungi a.k.a The Next Speaker-Baba Pilato!

Taarifa zinaonesha kuwa kwa nchi za Afrika Mashariki na Kati, Jamhuri ya watu wa Kenya ndio nchi ambayo ina mifumo inayo tekeleza Siasa huru na Demokrasia ya kiwango kizuri ukilinganishs na nchi zingine katika ukanda huo. Pamoja na kuwepo kwa Siasa za Ukanda na Makabila kwa muda mrefu lakini bado siasa zao zimekuwa ni za mfano kupita zetu za Tanzania.

Je, tunajifunza nini? kuna lipi unalo lijua kuhusu mfumo wao ambacho kwetu hakipo? Je, wananchi wao na wana siasa wao wana tabia gani ambazo ni tofauti na kwetu Tanzania? Saidia kujadili ili tupate Ufahamu.

KILA MTU ABEBE MZIGO WAKE….. LASIVYO, MWAFA! -Peter Sarungi

Peter Sarungi a.k.a The Next Speaker-Baba Pilato!

Naunga mkono kauli ya Mkuu wa Kaya kwa watani (Wajukuu) wangu wa mkoa wa kagera lakini naunga mkono kwa utani maana tulilia pamoja wakati wa msiba sasa ni lazima niwatanie kidogo kipindi hiki cha matanga.

Naamini hata Mkuu wa Kaya alikuwa anawatania ili kuwarudisha katika hali ya Kazi Tu ingawa bado sijafahamu kama Mkuu wa Kaya ni mtani wenu kikabila au kisiasa, naendelea kufanya utafiti kwa kina.

Huu ndio utani wa kisiasa, wanasiasa wana tabia ya kubadilika badilika kama walivyo wananchi wenyewe (No guarantee at all)Ni Utani tu kwa Wajukuu zangu, dont take seriousl

TANZANIA INAHITAJI MIFUMO IMARA KULIKO VIONGOZI IMARA- Peter Sarungi

Bara la Africa ni moja kati bara lililo wahi kutawaliwa na viongozi washupavu, majasiri na imara kwa muda mrefu bila mafanikio. Historia imeshuhudia viongozi jasiri na imara kama Mandela, Kwame Nkuruma, Gadafi, Idd Amini, Nyerere, Samwel Doo, Samora, Patrick Lumumba, Mugabe, Kawawa Simba wa vita, Mobutu Seseko, Savimbi, Karume, Kabila sr, Kenyatta sr, Obotte, Kagame, Satta na wengine wengi ambao walitikisa Afrika wakati wa utawala wao na wengine wapo mpaka sasa. Historia inaonesha kuwa watawala hawa walikuwa Imara ingawa wengine walitawala kwa mabavu, vita, mauaji ya alaiki na wengi walitawala nje ya mfumo wa demokrasia kupitia chama kimoja. Pamoja na uimara na ujasiri wa hawa viongozi bado Afrika imeendelea kulia na kuteseka na umasikini, maradhi na ujinga kwa viongozi na wananchi wao, Bado Afrika imeendelea kumwaga damu yao wenyewe kwa wenyewe, Bado Afrika imeendelea kuwa dhaifu kutokana na utengano dhidi ya mataifa ya magharibi na Asia, Bado Afrika imeendelea kuwa tegemezi katika afya, elimu, teknolojia, biashara, uchumi, utawala na mengi ambayo yanatoka nje ya afrika.

Tanzania tumebahatika kupata kiongozi imara, shupavu, jasiri na mwenye msimamo. Kiongozi anayeweza kufanya maamuzi na akasimamia maamuzi yake bila kutetereka hata kama yatakuwa na makosa, kiongozi anayethubutu kupita viongozi watatu waliopita. Huyu ni Dr John Pombe Magufuli (Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania), Mimi binafsi namkubali sana Mhe. JPM ingawa ana baadhi ya mapungufu kama binadamu lakini bado ameonesha kuwa yeye ni imara. JPM kwa sasa amekuwa ni gumzo kwa bara letu la Afrika na dunia kwa ujumla. Nimepata kuona taarifa nyingi sana kutoka nchi zingine Afrika na Duniani kuhusu uimara wa JPM na hata mwaka uliopita JPM amekuwa ni Raisi wa Afrika aliyejadiliwa na kupata umaarufu mkubwa kuliko maraisi wengine. Hii ni tunu na sifa nzuri kwa utawala wake.

Pamoja Uimara wa JPM, Bado Tanzania tumendelea kulia kilio cha uchumi duni, afya mbovu, elimu duni, demokrasia na udikteta, uhuru wa kujieleza, upatikanaji wa haki mahakamani, utawala bora, utumiaji wa nguvu na vitisho, wajibu wa bunge na wabunge, uelewa wa haki na wajibu wa raia, uchaguzi huru na wa haki, uzalendo na utaifa. Haya ni mambo yanayo endelea kurudisha nyuma maendelea ya taifa letu kwa kasi kubwa sana.

Hii ina sababishwa na Mifumo mibovu, kandamizi na yenye mianya ya kutenda maovu. Mifumo inatoa nguvu nyingi kwa kiongozi mmoja bila kuwa na njia za kudhibiti akikosea, mifumo inayo elekeza kiongozi kuwa juu ya sheria kwa kauli na matendo, mifumo inayo weza kuyumbishwa mda wowote bila kujali athari, mifumo inayo unganisha chama na serikali kuwa kitu kimoja, Mifumo tegemezi katika taasisi za nchi.

Hii mifumo mibovu ndio chanzo cha wana nchi kuendelea kulia vilia vilivyo zoeleka. Kwa aina ya mifumo hii, hata aje malaika kutoka mbinguni kuja kutawala bila kubadili ni sawa na kutwanga maji ndani ya kinu. Tunaweza kuwa viongozi imara kam JPM hata 50 lakini kwa mifumo yetu bado tutaendelea kuumia kila siku.

Peter Sarungi a.k.a The Next Speaker-Baba Pilato!

#MyTake

Bora kuwa na Mifumo imara itakayo weza kulinda maslahi ya nchi na wananchi wake hata kama kiongozi wa mfumo atakuwa legelege, bado mfumo utamnyoosha na kumlinda kuliko kuwa na kiongozi imara ndani ya mifumo dhaifu, maana siku kiongozi imara akibadilika basi nchi itarudi nyuma tena.

Mhe. JPM ni kiongozi Imara lakini mifumo ya serikali na taasisi zake bado zinaonesha udhaifu mkubwa na ndio maana utumbuaji ni mkubwa mno, Yaani kila kiongozi anayeguswa katika taasisi ni kama ameoza kwa rushwa, uzembe, uvivu na mengine mengi.

Tunahitaji mifumo imara kama ya jirani zetu Kenya na Zambia wanaoweza kusimamia matakwa ya wana nchi kisheria bila kutetereka.