All posts by Alpha Igogo

Kheri ya siku ya kuzaliwa kwa mama yangu mimi!

Leo kazaliwa mama yangu mzazi, kipenzi cha roho yangu! Kwabahati mbaya afya yake imeleta shida kidogo. Lakini pamoja na yote hayo bado twamrudishia Mungu shukrani zetu za dhati kwani anastahili sifa zote na utukufu mkuu!

kama anavyoonekana hapo kwenye hiyo video akiwa mnyonge, ni baada ya kutoka hospital. Na mzamini wa pendo lake akiwa amemletea zawadi ya saa mpya na simu. ??

“Tumefika nyumbani. Mzaliwa mpya, aliye mgonjwa tumemkuta anaendelea vyema. Kapokea zawadi za Birth Day toka kwa Baba/Babu/Mfadhili na rafiki.” …. Maneno yake mzee O.O Igogo baada ya Kufika nyumbani akitokea safari.

Wazazi wangu ni wapenzi wa saa za RADO! Hii ndio aina ya saaa toka na kuwa mpaka leo hii naona wanazivaa tu! Sijawahi kujua kwanini labda siku nidodose! ?? Sindio “upaparazi” wenyewe huo! ??

Happy birthday mama, tunakupenda sana, na tunakuombea afya njema. Birthday itarudiwa pindi mjukuu wako number moja akifika hapo kesho kutwa. Tunaamini Mungu atakuwa amesha kuponya. Amen!

Mwanangu mimi ….!

Unajua saa nyingine huwa siamini kama ni mwanangu ?? Mwenzenu nimekuza! Nikiangalia tulipotoka na tunapoelekea yani hakuna ninachokiona zaidi ya mkono wa Mungu ukiwa juu ya vichwa vyetu kumimina mibaraka yake.

Namshukuru Mungu sana na nitalitukuza jina lake milele. Kanipa rafiki wa milele. Tumekuwa pamoja, tumejifunza mengi pamoja, haswa kupitia makosa yangu mimi kama mama yake, yakampa somo la moja kwa moja. Mungu ni mwema sana. Nimevuka stage ya kuwa strictly mama; sasa hivi ni mama plus rafiki. Tunaongea na kuelekezana kirafiki tu! Kama malezi niliyompa kabla ya miaka 18 hayakumuingia na kumtengeneza kuwa kiumbe bora basi katika umri huu hakuna kitakacho mbadili zaidi ya kumuombea tu! Namshukuru Mungu sanaaaaaaa, mwanangu hajawai kunisumbua hata kidogo. Mungu kanibariki na mtoto msikivu, mwenye hofu ya Mungu, yani ni mtoto mwema mnoooo ndio maana saa nyingine siamini kama nimemlea mimi! ?? such a beautiful, humble, strong, smart, intelligent, classy, loyal, hard working, independent, charming young lady. I mean the list can go on and on but glory and honor all to Almighty God! ??

Leo nimejisikia kupost picha zetu haswa zahuyu mrembo wangu! ?? Kwani kunatatizo?! ?? sikuhizi nimeachana na kupost picha za watu haswa tusio na undugu, urafiki au mazoea. Ndio maana mnaniona sipost mara kwa mara. Nafanya mambo yangu mengine ambayo yananipa furaha na amani zaidi na hayo ndio nitakuwa napost humu.

??

Nimejisikia kumpost kuweka kumbukumbu ?? si blog ya mama yake jamani! ?? Ndio raha yakuwa na kitu chako mwenyewe ulicho kitengeneza wewe mwenyewe kwa utashi wa akili zako na mikono yako miwili. Hakuna atakaye kupangia nini cha kufanya labda huyo mtu ni punguani! ?? ………… Mungu azidi kumbariki sana na kumpa afya njema. ??

Sherehe ya maisha ya mwisho ya mama Yucabeth Atieno Chaulo!

Marehemu Mama Yucabeth Atieno Chaulo enzi ya uhai wake!

Siku ya Alhamisi ya tarehe 24, mwezi wa Sita, mwaka huu (06/24th/2021) familia ya marehemu mzee Androniko Chaulo walipatwa na msiba wa mama yetu Yucabeth Atieno Chaulo, kilichotokea mida saa mbili usiku huko Dar es salaam, Tanzania. Na amezikwa leo kwenye makaburi ya ukoo wa Chaulo yaliopo katika kijiji cha Buturi, wilaya ya Rorya mkoa wa Mara, ambako ndipo makazi ya kudumu ya ukoo wa Chaulo.

Pichani juu ni mama yangu mzazi (mwenye Tie dye) pamoja na marehemu. Mapema mwaka huu alipokwenda kutembelea makazi ya mama yangu huko Kibada, Dar es salaam.

Mama Yucabeth Atieno Chaulo ni mama mzazi wa Shemeji yangu mkubwa Mussa Chaulo a.k.a baba Danny. Shemeji Mussa amemuoa dada yangu mkubwa Elline Igogo a.k.a mama Danny takriban miaka 21 na miezi kadhaa sasa. Wamebahatika kupata watoto watatu Daniel, Chaulo, na Cecilia.

family!

Akiwa na baadhi ya watoto zake, wakwe zake, mama yangu mzazi, na mdogo wangu (mwenye darkblue), Kibada Dar es salaam.

Bahati mbaya miezi kama mitatu hivi iliyopita marehemu mama Yucabeth Atieno Chaulo alimzika mmoja wa binti zake ambaye yupo kwenye picha hii, (wapili kutoka kushoto mwa dada mwenye nguo Nyekundu, nyuma ya mama yangu naye amevaa Tie Dye)! ….. Roho zao zipumzike kwa amani ya Bwana.

Mama yetu alikua akisumbuliwa na mapafu kwa muda mrefu kidogo, alikuja Dar es salaam kwaajili ya matibabu na ndipo mauti ilipomkutia. Kwa asili yeye ni Mkenya (mzaliwa wa Kenya / mluo toka Kenya) ambaye aliolewa ujaluoni huko Buturi, na ndipo alipokua ameishi muda wote wa uhai wake.

Ibada ya kuuaga mwili , Dar es salaam

Beautiful and peaceful sendoff kwa mama yetu Yucabeth Chaulo yaliyofanyika nyumbani kwa mmoja wa watoto wake huko Mwanangati, Yombo Vituka, Dar es salaam. Kuishi maisha ya kumtukuza Mungu ni raha na amani tele! Amemaliza mwendo, tuonane asubuhi ile njema! ?? ……. Aneyeimba ni mwimbaji mashuhuri ajulikanaye kama Angela Magoti. Angela ameolewa na mjukuu wa marehemu.

“Nikasikia sauti kutoka mbinguni ikisema, Andika, Heri wafu wafao katika Bwana tangu sasa. Naam, asema Roho, wapate kupumzika baada ya taabu zao; kwa kuwa matendo yao yafuatana nao.” Ufunuo 14:13

Video hizi zote ni ibada ya mazishi yake leo hii 07/01/2021 huko Buturi, Rorya.

Video hii haina uhusiano na msiba huu! Japo wimbo wao huo ndio uliokuwa ukitumbuiza wafiwa.

“Bali wewe, uwe na kiasi katika mambo yote, vumilia mabaya, fanya kazi ya mhubiri wa Injili, timiliza huduma yako. Kwa maana, mimi sasa namiminwa, na wakati wa kufariki kwangu umefika. Nimevipiga vita vilivyo vizuri, mwendo nimeumaliza, Imani nimeilinda; Baada ya hayo nimewekewa taji ya haki, ambayo Bwana, mhukumu mwenye haki, atanipa siku ile; wala si mimi tu, bali na watu wote pia waliopenda kufunuliwa kwake.” 2Timothy 4:5-8

Bwana alitoa na Bwana ametwaa jina lake lihimidiwe milele zote. Tuonane Paradiso mama yetu! ????

Video hii haina uhusiano wowote na msiba.

Kheri ya siku ya kuzaliwa kwetu!

Siku ya leo mika zaidi ya arobaini iliyopita nilizaliwa mrembo mimi! ?

Namshukuru Mungu kwa kunipa kibali cha kuona mwaka mwingine!

Namuomba azidi kunishika mkono katika mwaka huu kama ulivyofanya mwazo! ????

Naamini nimejiandaa kadri ya uwezo wangu katika umri huu mpya. Nimesafisha uchafu karibia wote katika kila kona ya maisha yangu! Nimefanya maamuzi ambayo mimi mwenyewe nikikaa chini nasikia furaha moyoni mwangu! Fake friends nimewapa mkono wa kwaheri! Bila chuki wala hiyana! Well! No one cries when fake friends say goodbye! Ni Xmas tuu to me! ??

Kuna mpumbavu mmoja (excuse my language) kwa muda sana alikua anazunguka kupandikiza chuki juu yangu, kapandikiza chuki kweli kweli! Lakini hakujua kua kuna Mungu, na kwa uwezo wa Mungu mwaka huu nimetuliza. Mwanzoni nimetamani sana kumpeleka kwenye vyombo vya sheria, lakini nimeamua kumpuuza! Nimemuachia Mungu atajua nini chakumfanya!

New age, New soul, New attitude! Ni mwendo wa #Kanyaga kwakwenda mbele! Nimeshaucheza huu wimbo zaidi ya mara 20 wiki hii! ?? I am truly feeling it! Yani kitu kikinikera nasitaki kukipa my attention naimba tu #Kanyaga halafu najikuta naachana nacho! ???? ….. Namshukuru Mungu kwa yote! Happy birthday to me!

Pia leo amezaliwa mrembo Dia Alex Odemba! Naye twamshukuru Mungu kwa mibaraka yake! Happy birthday to her!

Zifuatazo ni salamu kutoka kwa baadhi ya ndugu!

Happy birthday to us! ????

“Yesterday I was in that meeting as from 8 am till 4.30 pm, Chaired by Her Excellency President Samia Suluhu Hassan. Then today we were in the meeting Chaired by the Hon. Prime Minister, Majaliwa Kassim Majaliwa, as from 9.00am till at 4.30 pm. No wonder I forgot to Congratulate you timely.??‍♀️

BELATED Birth Day Greetings. Better LATE, than NEVER. It was yesterday, when you counted another additional 365 days after your last Anniversary, that makes you more healthier spritualy and emotionaly. We are proud that as we age down to our seventies, you are as well aging up to become our care taker, a daughter in America whom we shall be Visting and staying with at her place, to share the little blessings of her with abundat Love from her inner heart, as we do Love her. Arwa Nyangaji, Dani Min Rhoda Nyolwengo aka “Agali Nyogot” Take Our Late birthday Wishes, knowing that we are aging down and becoming more forgetfull. Baba & Mama.”

Sherehe ya kipekee ya kumuaga Dorice Sassi Igogo!

Ameagwa rasmi! Siku ya Jumatano, tarehe 06/02/2021 zilisikika nderemo na vigelegele vingi sana kutoka kwa familia ya Mr. Emmanuel Agonda Sassi (marehemu) na Mrs. Magreth Cornel Awiti a..k.a Mrs Agonda, a.k.a Mrs Sassi pamoja na wanaukoo wote wa Adol Igogo. Ilikuwa ni furaha ya kumuaga rasmi binti yao kipenzi Mwalimu Dorice Sassi Igogo ambaye anakwenda kuanzisha rasmi kaya (familia) yake.

Dorice akiwa na mtarajiwa wake

Ndoa ni jambo la kheri, ndio maana wazazi hufanya sherehe ya kipekee kabisa ili kumuaga mpendwa wao, kama njia mojawapo ya kuonyesha furaha yao na shukrani kwa Mungu.

Dorice a.k.a Vumilia ni binti aliyezaliwa katika familia ya watoto (3) watatu, yeye akiwa mtoto wa pili kuzaliwa na msichana pekee.

Mtoto wa kwanza ni Yustor Sassi (Kulia), Dorice, na Joseph (kushoto). Katika picha hii inaonyesha makaka wakimlisha keki dada yao, na mama mzazi akiwa pembeni anaangalia.

Yustor akiwa nafuraha nyingi wakati wa kulishwa keki na dada yake.

Joseph naye akifurahia kulishwa keki na dada

Yustor akimpigia saluti mdogo wake, kwa heshima kubwa kama afanyavyo huko jeshini!

Tazama jinsi kaka wa bibi harusi mtarajiwa akitoa saluti kwa mdogo wake kwa furaha na ushupavu wa kijeshi.

Bibi harusi mtarajiwa akielezea historia yao, wapi walikutana na nini kiliwakutanisha.

Zawadi kwa bwanaharusi mtarajiwa

Bibi harusi mtarajiwa akiwa na Mc wa shughuli hiyo ajulikanaye kama McKatokisha

Wamazazi wa upande wa bibi harusi mtarajiwa

Yani mdogo wangu huyu kwa kuchakarika aaah! Ni Mwalimu na pia ni mjasiriamali wa nguvu. Hii keki ametengeneza mwenyewe kwa mikono yake kupitia kampuni yake ya isadoricakes and sassyjuice! Izidi barikiwa kazi ya mikono yake.

Mtarajiwa akikata keki

Akilimlisha mama mzazi kwa unyenyekevu na upendo mwingi

Akimpatia mama mzaa chema keki yake kama ishara ya upendo na ukarimu wake kwake na ukoo wa mumewe mtarajiwa.

Mama mzazi naye alipata kipande chake

Mama wazaa chema na binti yao

Wamependeza kwakweli

Haya ngoja nikusaidie kidogo kama haujui, bibi harusi mtarajiwa ni mtoto wa mama yangu mdogo. Mama yake ndio kitinda mimba kwa uzao wa bibi yangu mzaa mama. Sasa basi, kama ilivyo kwa mama yake Geoffrey Kateti (kama mnamkumbuka) ndivyo ilivyo kwa mama yake na bidada hapa. Mama yake naye alifuata nyayo za dada yake (mama yangu) akaolewa Utegi! Utegi oyeeee! ?? Tofauti na mama yake Geoffrey, mama yake Dorice ameolewa ukoo mmoja na dada yake ?? chezea ukoo wa Odol! Hivyo Dorice ni mdogo wangu pande zote; kwa baba na kwa mama.

Mapenzi ya Mungu yalitimizwa baba yangu mdogo (baba wa bibi harusi mtarajiwa) aitwae Emmanuel Agonda Sassi, alishalala usingizi wa mauti takriban miaka 4 iliyopita. Twamshukuru Mungu kwa yote.

Once again, hongera sana mdogo wangu, shemeji tunakukaribisha kwetu kwa mikono miwili. Mungu awe nanyi siku zote. Amen! ????

?@lush___makeup

? @mckatokisha

? Decor@lillies_luxe_decor

#FBF

Embu tujikumbushie mambo yalivyo kuwa siku ya kuvikana Pete ya ahadi ya ndoa /uchumba, siku ya Jumatatu ya mwezi wa kwanza tarehe kumi na mbili mwaka huu, 01/12/2021. Love is the beautiful thing.

Sherehe ya kuagwa kwa Rhoda Igogo!

Siku ya Jumapili ya tarehe 05/23/2021 ndio ilikuwa siku rasmi ya kuagwa kwa bibi Rhoda Alexander Igogo. Sherehe hiyo ilifanyika nyumbani kwa baba yake mlezi huko Segerea. Zifuatazo ni baadhi ya picha na video kutoka kwenye tukio hilo. Picha hazipo kwenye mpangilio rasmi nimeweka tu!

Bibi harusi mtarajiwa akiingia ukumbuni

Mr Victor na mkewe mtarajiwa!

Rhoda na mpambe wake bi. Oliver Chumo

Oliver

Baba mubwa wa Rhoda, mzee Charles Olung’a Igogo

Wazazi wa bwana harusi mtarajiwa, Mr and Mrs Ollal

Wanandoa wapya Mr and Mrs Isaka Alexander Igogo

Mama mdogo wa Rhoda, Mrs O.O Igogo akipungia wageni

Baba mkubwa wa Rhoda, mzee Charles Olung’a Igogo (kushoto) pamoja na baba mlezi mzee O.O Igogo

Dada wa bwanaharusi mtarajiwa Ms. Aphino Alexander Igogo, pamoja na mdogo wa bibi harusi mtarajiwa Blessing Igogo wakimkaribisha shemeji yao kwa furaha.

Rhoda na mama yake mzazi

Bwanaharusi mtarajiwa akiwa na bibi yake mzaa mama yake.

wageni waalikwa wakiwa na mwenyeji wao mzee O.O Igogo

Mc Rhevan katika ubora wake

Bibi harusi mtarajiwa number 2 akitoa ombi la mwisho.

Rhoda akitoa zawadi ya keki kwa Mkurugenzi Mkuu wa Utegi Technical Ltd, Mrs Margaret Mabada kwa niaba ya wafanyakazi wote wa Utegi ambapo Rhoda ameajiriwa.

Rhoda akicheze na wafanyakazi wenzake

Baba na binti yake wakicheza

Kwa picha zaidi bonyeza ????

https://RHEVANSTUDIO2021.pixieset.com/rhodasendoffpartyphotos/

Kitchen party ya RHoda Igogo

Bibi harusi mtarajiwa Rhoda Alexander Igogo

Wakati tukisubiria picha kutoka kwa wataalamu waliolipwa kufanya kazi hiyo, basi tuanze na tulizonazo.

Siku ya jumapili tarehe 05 /16 /2021 ilifanyika sherehe ya kumfunda mwali (bibi harusi mtarajiwa) a.k.a Kitchen party ya Rhoda Alexander Igogo. Sherehe hii aliandaliwa na mama yake mlezi akishirikiana na ndugu na jamaa pamoja na marafiki. Ilifanyika kwenye makazi ya wazazi walezi huko Segerea ambapo bibi harusi mtarajiwa ndipo anapo ishi na ndipo atakapotokea kwenda kwa mwenza wake.

Akiingia ukumbuni mwenye nyuso ya furaha na tabasamu kama lote ndio mama mzazi wa Rhoda na Isaka, Mrs Joyce Alexander Igogo. Ni mke wa marehemu baba yangu mkubwa (wapili kuzaliwa kwenye familia yao baba, watoto bibi Rhoda Nyakanga Olwengo). Babu yangu mzaa baba (Marehemu mzee William Olung’a Igogo) alikuwa na wake watano (5) ??? usishangae sana maana marehemu babu yake baba (my great grandfather) Chief Sarungi Igogo yeye alikuwa na wake 19 ??????? welcome to our ukoo ?? …… Rhoda ndio mtoto wa mwisho kwao. Akitoka kuzaliwa Isaka ndio Rhoda anafuata. Na harusi zao zimekuwa ndani ya mwezi mmoja. Familia hii inajumla ya watoto 7 walio hai, mmoja alifariki. Grace a.k.a Anyango, Aphino a.k.a Nyawade, Kenneth (Marehemu) a.k.a Ukombozi, William a.k.a Mzee, Dr. Obadiah, Isaka, na Rhoda a.k.a Nyolwengo, na Emilia Igogo! ….. Mungu ni mwema sana.


Haya embu tufurahishe macho kwa hizi tilizonazo!

Pichani ni Dia Alex Odemba na bibi yake mama Igogo.

Dada kama dada! Huyu ni dada yake Rhoda aitwae Aphino.

Dia Alex Odemba katika ubora wake!

Mama wa isadoricakes_and_sassyjuice. Dogo langu Mwalimu mwenye ujasiriamali wake! ??

bibi harusi mtarajiwa akikata cake yake

Kwamahitaji yako ya Cake nzuri zenye ubora wake, juice fresh tamu, na Mc wa kitchen party, tafadhali husisite kumtafuta @isadoricakes_and_sassyjuice ndio habari ya taifa! ???

Kutoka kushoto ni mama yangu mzazi, akifuatiwa na mdogo wangu Vumi Sassi, anayefuata ni mdogo wake mama yangu (kitinda mimba kwa familia yao) napia ni mama yake Vumi aitwaye Magreth Cornel Awiti a.k.a Mrs Agonda Sassi, na anayefuata ni mdogo wangu kipenzi Magreth Rhoda-Nyasungu a.k.a Mrs Massawe.

?? mama zangu hao! ??

Rhoda akiingia ukumbini kwa furaha kabisa

Mama mlezi wa Rhoda

Mrs Vetto Igogo (kushoto) pamoja na Mrs Isaka Igogo (kulia). Mmemuona bibi harusi wetu wa wiki iliyopita?! ?? Miguu imeiona? Miguu halisi ya Kiafrika! Yani wana miguu ya bia kama mawifi zao! ??

Baba naye hakutaka kupitwa na matukio katika picha ?? akiwa na furaha kubwa pamoja na binti zake akitaniana na ucheshi wa hapa na pale.

Mtu na wifi zake! Mrs. Massawe kwa mbele hapo, Mrs Vetto Igogo mtu kati, na Mrs Isaka Igogo nyuma hapo.

Wifi karibu sana Utegi!

Watu wakiserebuka kwa raha zao!

Mke ya Mrombo! ??

Mwenye nguo ya njano, anayecheza kwa hisia zote, ni dada wa bibi harusi mtarajiwa, aitwaye Grace Alexander Igogo a.k.a Anyango, yeye ndio mzaliwa wa kwanza kwa familia yao. Anafurahia kusindikiza kitinda mimba kuanzisha familia yake. Pembeni yake ni mama mlezi wa Rhoda.

Mama naye hakutaka kujivunga kwani wimbo wenyewe siunausikia? ???

Haya tunamtakia Rhoda safari njema katika kuhitimisha kilele cha sherehe za kuagwa kwake na familia yake mpaka siku ya harusi. Jumapili hii ni Send-off yake na Jumapili ijayo ndio harusi. Mungu awatangulie katika kila jambo!

BTW, hii siyo mara yakwanza kwa familia yetu kuwa na harusi mbili kwa mpigo (double wedding), kaka yangu mkubwa Vetto Igogo na dada yangu Elline Igogo harusi zao zilipishana wiki tu, tuliserebuka kwa wiki mbili mfululizo! Yani tulianza na kitchen party ya dada Elline, ikafuta harusi ya kaka Vetto, ikaja Send-off party ya dada Elline kisha harusi yake. Na baada ya hapo ikafuata sherehe ya kuvunja kamati. ??? I tell you, this familia loves to partyyy! Nahiyo ni miaka ishirini na mbili (22 yrs ago) iliyopita. Na sherehe zao Ilikuwa kubwa kweli kweli hizi ni chamtoto! Mama zigi-zig catering na Dotnata Catering walipika mpaka walishangaa. ???

***Updates: picha za nyongeza***

Rhoda na binamu yake Honorable Madam Judge Dr Modesta Opiyo.

Rhoda na mama yake mzazi

Juu ni mama mkwe wake Rhoda Mrs Scola Oguna Ollal.

Mawaidha ya akina mama, shangazi, na wanawake wachanga kwenye ndoa.

Mama mdogo Mrs O.O Igogo akitoa ombi la kwanza.

Mama mdogo Mrs Agonda Sassi akitoa ombi la mwisho. Walianza na Mungu wakamaliza na Mungu. Amen!

Kwa picha zaidi bonyeza ????

https://RHEVANSTUDIO2021.pixieset.com/pendokitchenpartyphotos/

Rhoda na rafiki yake, hizi ni pre-wedding pictures

Blessing latika ubora wake

Wadada hao! ??

Kwa picha zaidi bonyeza ????

https://RHEVANSTUDIO2021.pixieset.com/rhodapresendoffphotos/

NYONGEZA: HARUSI YA ISAKA NA SARAH.

Video hapo juu ni muhtasari wa harusi ya Isaka na Sarah, imetengenezwa na studio za Mc Rhevan.

Mr and Mrs Jacob Massawe

Zifuatazo ni baadhi ya picha za ziada na video zilizotengenezwa na camera binafsi za wanandugu. Naziweka humu ili ziwe sehemu ya kumbukumbu. …… Hapo juu ni dada wa bwanaharusi Magreth Rhoda-Nyasungu a k.a Magreth Otieno Igogo a.k.a Mrs Massawe akiwa sambamba na laazizi wake ambaye ni Shemeji wa bwanaharusi. #Warombo #SweetMangi ??

Mama Dia a.k.a Cheusi akiwa na best ake mama Igogo

Dia Alex Odemba akideka kwa bibi yake.

Mrs. Massawe

Shemeji yake Isaka, Mr. Massawe (kushoto) akiwa na kaka zake Isaka, Mr. Albetus Ajee Chuche (mtu kati) na Mr. Guka Otieno Igogo (kulia).

Mashabiki wa Simba nao walipewa haki yao! ?

Hongera sana Isaka na Sarah!

Mr and Mrs Isaka Alexander Olung’a Igogo

Hayawi hayawi sasa yamekuwa! Wamehalalishwa duniani na Mbinguni yakwamba wawili hawa ni mwili mmoja!

Sarah akila kiapo kitakatifu

Agano hili takatifu lilifanyika siku ya Jumosi tarehe 05 /08/2021 katika kanisa la viziwi lililopo huko Bunguruni, Dar es salaam. Tunawaombe baraka nyingi sana katika familia yao hii mpya walio ianzisha!

Bibi harusi

Bwanaharusi akihakikisha je kweli ni yeye?! Kabla ya kula kiapo, maana hukawii kubadilishiwa mke kama Jacob (Yakobo)! ? mjini mambo mengi jama! ?

Bwanaharusi amehakikisha na ameridhia! ?? Kama hujawahi sikia kisa cha Jacob (Yakobo) basi chukua Biblia yako na ufungue kitabu cha mwanzo sura 29 yote itakupa stori kamili!

Kwaufupi ni kwamba, Jacob baada ya kutumikia miaka saba kwa mzee Labani kama mahari ya kumuoa binti yake Rachel (Raheli), siku ya harusi akakuta amebadilishiwa mke anaye mpenda kwa dhati na kupewa Lea ambaye alikuwa ni dada wa Rachel (Raheli). Kwani kulingana na mila na desturi za kabila na ukoo wa mzee Labani ni kuwa mkubwa lazima aolewe kwanza ndipo mdogo anafuata. Kwa maana hiyo Jacob ilibidi atumikie miaka 7 mingine ili aweze kumpata Rachel. Kwa maana hiyo Jacob alitumikia miaka 14 kwa mzee Labani kama mahari ya kumuoa kipenzi cha roho yake! …… Sikilizeni wanawake wenzangu, kama mwanaume anakupenda basi hakuna gumu wala zito mbele ya macho yake! He will move mountains just to have you! Tena bila hiyana yoyote! Wanawake wazuri ni wengi sana lakini Mke ni mmoja tu ambaye kila mwanaume anajua hilo!

Maharusi na wapambe wao
Wasimamizi wao
Mchungaji aliye idhinisha ndoa hii

Sarah akisindikizwa na kaka yake aitwaye Alex ambaye ndiye aliyemlea toka wazazi wake wamefariki hadi leo hii anapokwenda kuanzisha nyumba yake mwenyewe. Kwa Sarah hamuoni Alex kama kaka bali ni baba yake mlezi na mke wa Alex ni mama yake mlezi, hao ndio wazazi wa Sarah.

Hapo juu ni baba mlezi wa Isaka ajulikanaye kama mzee O.O Igogo. Yeye ndio amemlea Isaka toka akiwa na miaka 5. Baba mzazi wa Isaka amefariki takribani miaka 7 iliyopita. Mzee 0tieno Igogo ni mdogo wake na marehemu mzee Alexander Igogo ambaye ndiyo Baba yake na Isaka.

Mama mlezi wa Isaka Mrs O.O Igogo akisalimia maharusi, nyuma yake ni mjukuu wake aitwaye Essy.

Mashangazi na mama wakubwa kwa wadogo upande wa bwanaharusi.

Baba mlezi akiwa na furaha nyingi usoni kwa kuongeza mtoto mwingine kwa familia.

Madada, mabinamu, na mashemeji wakiingia kwa shangwe!

Kutoka kulia, ni mdogo wa bwanaharusi aitwaye Blessing, akifuatiwa na mpwa (niece) wa bwanaharusi Essy, akifuatiwa na shemeji mkubwa Mrs. Vetto Igogo, na dada mkubwa (wapili kuzaliwa kwenye familia ya kina Isaka) Aphino Alexander Igogo (Mrs Ogoche).

Mdada mwenye nguo ya blue kutoka kushoto, huyo ndio kitinda mimba kwenye familia ya akina Isaka. Anaitwa Rhoda Alexander Igogo. Naye harusi yake ni mwishoni mwa mwezi huu. Wiki hii ni kitchen party yake.

Bibi harusi mtarajiwa Rhoda Alexander Igogo akiwa na maharusi Mr and Mrs Isaka Alexander Igogo.

Bibi harusi mtarajiwa, bi Rhoda akifurahia kaka kupata “jiko”!

Mama mlezi wa bwana harusi pamoja na baba msimamizi wa ndoa hii mzee Samuel Olung’a Igogo wakitoa nasaha zao.

Baba mlezi akitoa neno kwa niaba ya kamati!

Mama mlezi akiwa na maharusi

Maharusi wakikata keki!

Wapendwa, kwamahitaji yako ya Cake nzuri zenye ubora wake, juice fresh tamu, na Mc wa kitchen party, tafadhali husisite kumtafuta @isadoricakes_and_sassyjuice ndio habari ya taifa! ???

nnnnn

Maharusi wakifungua dancing floor kwa kucheza ziro-diatance music ?? asiye na wake akumbatie chupa ya soda! ???

Meza kuu upande wa bibi harusi

The Olung’as!

Hawa ni baba zake Isaka, wadogo kwa wakubwa. Kutoka kushoto ambaye kichwa tu ndio kimeonekana ni mzee Samuel Olung’a Igogo (baba mkubwa na msimamizi wa ndoa hii), akifuatiwa na mzee Charles Olung’a Igogo (baba mkubwa), akifuatiwa na mzee Otieno Olung’a Igogo (baba mdogo na mlezi wa Isaka), akifuatiwa na Genga Olung’a Igogo (baba mdogo)

Walianza na Mungu, wakamaliza na Mungu. Mama mdogo wa Bwanaharusi Mrs Emmanuel Agonda Sassi Igogo akitoa sala ya mwisho!

Mathayo 19:5 “akasema, Kwa sababu hiyo, mtu atamwacha babaye na mamaye, ataambatana na mkewe; na hao wawili watakuwa mwili mmoja”!

Marko 10:9 “Basi, alichokiunganisha Mungu mwanadamu asikitenganishe” ….. I present to you Mr and Mrs Isaka Alexander Olung’a Igogo

Mc Rhevan mtu kati hapo

picha zote shukrani kwa Mc Rhevan studio. Ukitaka kuona picha za tukio nzima tembelea ????https://RHEVANSTUDIO2021.pixieset.com/isakaandsarahweddingphotos/

Tunawaombea kheri na baraka nyingi!

Bwana harusi mtarajiwa-Isaka akiwa kwenye pozi na bibi harusi mtarajiwa-Sarah

Kesho ndio siku yenyewe kuu, ambapo wawili hawa wataunganishwa kuwa kitu kimoja na koo mbili zitaunganishwa rasmi mbele za Mungu.

Naam, kwamara nyingine tena tunapenda kutoa pongezi nyingi sana kwa watarajiwa hawa kwa kufanya maamuzi mazito yenye busara. Mungu azidi kuwatangulia katika kila jambo ambalo limepangwa kufanyika kesho basi likapatae kibali mbele ya uso wa Bwana na lifanyike kama lilivyopangwa kwa utukufu wa Mungu.

Mwenyezi Mungu mwenye wingi wa rehema na neema awazidishie ulinzi wake na mibaraka yake siku zote za maisha yao. Ndoa yao ikajae amani na furaha, naye Mungu Baba awe mgeni wao siku zote. Wakabarikiwe wao na uzao wao wote. Twaomba kwa imani katika jina la Yesu. Amen! ????

akasema, Kwa sababu hiyo, mtu atamwacha babaye na mamaye, ataambatana na mkewe; na hao wawili watakuwa mwili mmoja!” *** Matayo 19:5

“Kwa sababu hiyo mtu atamwacha babaye na mamaye, ataambatana na mkewe” ****Marko 10:7

Jana ilikuwa siku ya kuagwa kwa bibi harusi mtarajiwa. Bi. Sarah alifiwa na wazazi wake wote wawili akiwa mdogo. Kaka yake Alex akamlea hadi sasa anatokea kwao kwenda kwake na mumewe mtarajiwa. Ni mlemavu wa kusikia na kusema??‍♂️ Hapo anatoa shukrani zake za moyoni kwa walezi wake siku ya kuagwa, na kuwapa zawadi alizomudu kama ishara ya shukrani na kumbukumbu. Mume wake mtarajiwa naye ana historia inayotaka kufanana na yake! Hawa wawili ni kielelezo halisi na ushuda hai kwamba kazi ya Mungu haina makosa.

Mimina neema zako Bwana mimina ????

??? mnaona mama zangu na shangazi yangu aliyegoma kuzeeka pale nyuma na tabasamu kama lote wakikumbushia enzi zao?! ?? so sweet!

Wababa nao hawakubaki nyuma! ??

Picha zote shukrani kwa Mc Rhevan , mtembelee Instagram @mc_Rhevan au website yake ???? https://mc.rhevan.com/

Nyumbani kumenogaaa …….!

Jamani-Jamani! Nyumbani kumenogaaa! Kama ilivyokua kawaida yao basi wametia timu tena!?? Mashangazi kwa wajomba, mama wadogo kwa wakubwa, baba wadogo kwa wakubwa, makaka kwa madada, bila kusahau mashemeji.

Si wengine bali ni familia ya marehemu Mzee William Olung’a Igogo wa Utegi, Rorya leo wamejumuika nyumbani kwa mzee O.O Igogo huko Segerea, Dar es salaam kwa maandalizi ya ndoa ya kijana wao ambaye ni mmoja wa wajukuu wa marehemu mzee William Olung’a Igogo ajulikanaye kama Isaka Alexander Igogo itakayo fanyika siku ya Jumosi tarehe 05 /08 / 2021, Dar es salaam, Tanzania.

Pichani juu ni maharusi watarajiwa bwana Isaka na Bi. Sarah katika pozi!

Basi, nami dada mtu napenda kuwatakia ndugu zangu kila la kheri katika hatua zilizo baki katika kutengeneza historia nyingine tena ya kuanzishwa kwa familia ya Bwana Isaka na Bi Sarah! Mungu awe azidi wabariki na atembee nanyi mpaka mwisho wa jukumu hili muhimu sana la kuunganisha koo mbili kua kitu kimoja! …. Nasikitika sijaweza kushiriki nanyi lakini nipo nanyi kiroho na kifikra! …. BTW, kwa msiofahamu udugu wangu na bwana harusi mtarajiwa ni hivi; Isaka ni mdogo wangu, yeye ni mtoto wa marehemu baba yangu mkubwa Alexander Olung’a Igogo. Baba yake ni mtoto wa pili kuzaliwa kwenye tumbo la bibi yangu akifuatiwa na baba yangu. Isaka alizaliwa na ulemavu wa kusikia na kuongea (kiziwi na pia ni bubu), hivyo kutoka na changamoto hizo baba yangu alimchukua na kumleta kuishi nasi Dar es salaam toka akiwa na miaka 5! Hiyo ilikuwa kwa madhumuni ya kumsaidia aweze kukaa karibu na wataalamu wenye ubobezi wa matatizo yake pia aweze kupata elimu stahiki!. Wengi wasiotufahamu vizuri huwa wanafikiria ni mtoto wa baba yangu kwasababu amekulia kwetu toka akiwa na umri huo. Ukweli ni mtoto wa kaka yake baba.

Mbarikiwe wote!

Ramadan Mubarak!

Kheri na baraka ya mfungo wa Ramadan kwa ndugu zangu, marafiki, na wafuasi wangu wote ambao ni waumini wa dini ya Uislamu. Mbarikiwe sana. ❤

Ramadan Mubarak to all my Muslim family members, friends, and fans! May it be Joyful and glorious! ❤

R.I.E.P uncle Zou Fu!

As family of O.O Igogo, we mourn the tragic death of our best friend, business partner, and family friend Sir. ZOU FU QIANG (in dark-red Tshirt) that happened in China earlier today! Our prayers go out to his family, friends, and everyone who is touched by his death!

From left Mr Molnar, Mr Igogo, and late Mr Zou

Mr Zou Fu a.k.a uncle Zou, he was one of the three founders and Shareholders of the on coming giant multi-millions Usd Copper Smelter and Gold Refinery entity, IGOZOMO ( IGOGO – ZOU – MOLNAR) Minerals Company Ltd, located in Mpwapwa district in Dodoma region, Tanzania.

2019 at Saba saba grounds!

Also, he was the owner and founder of Aloe vera herbal drug (Jufeel Aloe Vera juice) for human body immune boosting ……. Great human being to say the least! Such a beautiful soul gone too soon! We will surely miss you greatly!.????

“Rafiki yangu wa KWELI KIKWELI KWELI. MAREHEMU ZOU FU QIANG.(PUMZKA SALAMA.) MY DEAREST AND TRUETH FRIEND LATE Mr. ZOU FU QIANG. (REST IN PEACE)” by longtime best friend, brother, and business partner sir O.O Igogo.

Words of sympathy from Magreth
Words of sympathy from Magreth
Words of sympathy from Janet

“Thank you so much Arwa. That is a man who made me so popular and higly respected in the Chinese Communities, He was very loyal, honest, hard working, creative, excessfully kind to me and our family. I fail to stop crying whenever I recall his helping hand to all that I have gained since knowing him in 21 years. Let all of us in the family keep on praying for his Soul to rest in peace.???” ….. shukrani za baba kwa bintie Alpha kwa kutengeneza video ya baadhi ya matukio ya hivi karibuni ambayo marehemu alishiriki nasi.

Happy birthday Mercy!

Leo ni siku kazaliwa mrembo wangu! Alizaliwa siku ya JumaMosi kuu (siku moja kabla ya Pasaka). Saa tisa mchana katika hospital ya Tanzania Matertenity Service (Siku hizi inaitwa Tanzania Matertenity Hospital), chini ya uangalizi wa marehemu Dr Amood na Dr Kapesa.

Mercy!

Kalinitesa na uchungu haka, sitokaa nisahau! ?? Niliwekewa chupa mbili za maji ya uchungu ndipo kakatoka! ?? Alikuwa kanona ndani ya tumbo la mama yake na mama mwenye alikuwa na mwili mdogo. Nilikuwa napenda kula chips na kachumbari kupita maelezo! Yani ndio kilikuwa chakula changu kikuu kila usiku! Maharage yalikuwa hayapitiii, yani nikijilazimisha kula natapika bila kujijua! ?? Halafu utamsikia mama Igogo akisema “vipi? Mjukuu kakataa maharage?” ???

Namshukuru Mungu kwa zawadi ya hichi kiumbe! Nilizaa mtoto mwenye afya njema nikampa jina Mercy. Jina hili nilikuwa inspired na rafiki yangu ambaye tulisoma naye Kowak Girls Secondary school, yeye anaitwa Mercy Msofe, kwasasa anaishi Arusha. Pia anajina lingine ambalo alipewa na babu yake (baba yangu mzazi), alimpa jina la Theresia a.k.a Teddy. Nijina la marehemu shangazi yangu. Baba yangu kwao (tumbo la mama yake) walizaliwa wavulana watatu na msichana mmoja. Kwakua Mercy ndio mjukuu wa kwanza kwa wazazi wangu akaamua kumuenzi marehemu dada yake ambaye alifariki mwaka mmoja kabla ya Mercy kuzaliwa. Basi Mercy na Teddy yote ni majina yake. Na lakilugha ni Obworo! Ni nickname ya marehemu shangazi yangu, Theresia Obworo!

Mimi namuombea maisha mazuri sana yaliyojaa baraka nyingi na utukufu wa Bwana Mungu. Mwenyezi Mungu amuhepushe na pepo zote. Akalitukuze jina la Muumba wake siku zote za maisha yake. Naomba kwa imani katika jina la Yesu, Amen!

Happy birthday beautiful girl, nakupenda sana nawe wajua hivyo! ?❤

Zifuatazo ni baadhi ya salamu za kheri kutoka kwa :-

Kutoka kwa babu!

“Me & U, are 41 years older and younger than one another, that is what inspired me to wait until all has exhausted their best wishes to you on this very special day, when you have seen the 27th anniversry. As I strive to reach my 95th anniversary to come, my wishes are that you shall celebrate 68th anniversay while healthier with sound knowledge, richer in heart, wealthier in charity, and sorrounded with numerous loving family members as it is with me today, on this wonderfull good friday which filled with happiness of sharing my love with you. UWE NA SIKU MURUA SANA, AHEROI MOKALO NYAKWARA MOKUONGO. ☝️? With all my Love?From ? Babu.”

Aunt Janeth!
Kutoka kwa aunt Mage
Kutoka kwa cousin-sister Sarah

Happy birthday Mercy!

Happy birthday baba!

Leo ni siku kazaliwa mzee O.O Igogo wengine umuita mzee wa Utegi Tech! Na wanawe walimpa jina la utani “mzee wa pamba”! ?? Amegonga miaka 68 leo. Tunamtakia maisha marefu zaidi, mema sana, na yenye baraka nyingi sana. Happy birthday to him. ……. zifuatazo ni salamu kutoka baadhi ya watoto na wajukuu!

Ujumbe toka kwa binti yake, Alpha.

Baba naye akafurahia picha iliyoambatanishwa na salamu za kuzaliwa kwake, ?? I made him smile yeah! ??

Ujumbe toka kwa binti yake Janeth

Salamu za upendo toka kwa mjukuu Sarah, a.k.a Katuko Nyandege

Mziwanda nae hakubaki nyuma! Yeye kampiga picha na kuandika salamu kwa juu! ? smart girl!

Cake maalum kwa ajili ya babu! ??

Salamu kutoka kwa binti yake Magreth Rhoda-Nyasungu

Salamu kutoka kwa mjukuu number moja, Mercy!

Well, kwamara nyingine twamtakia kheri ya maisha marefu! ……. embu tuwakumbishie enzi zake wakati wa ujana wake ??

Mjaluo kama mjaluo! OG from Rorya! ??? Eti dad ake nani huyu?! Kweli umaridadi huficha umasikini! ??

#HappyBirthdayDad. #FBS

Tanzia: pumzika kwa amani ya Bwana baba mkubwa mzee John Obure!

Marehemu mzee John Obure enzi za uhai wake

Kwaniaba ya familia ya Mr and Mrs O.O Igogo naomba kuchukua nafasi hii kutoa salamu zetu za pole kwa familia ya marehemu mzee John Obure na Mwalimu Anna Cornel Awiti a.k.a Mrs John Obure, kilichotokea alfajiri ya leo huko Mwanza, Tanzania. Tunawaombea utulivu na amani wakati wote wa maombolezo wa msiba huu wa baba na Mungu akaendelee kuwa nguzo imara na kimbilio lenu wakati wote. Mwenyezi Mungu akawe mfariji wenu siku zote. Sisi sote tu mavumbi na mavumbini tutarudi!

Kwa faida ya wasomaji wangu, marehemu mzee John Obure ni baba yangu mkubwa. Yeye alimuoa mama yangu mkubwa ajulikanaye kama Mwalimu Anna Cornel Awiti. Wao maisha yao yote yalikuwa Musoma, na miaka ya hivi karibuni walihamia kijiji cha Shirati kilichopo wilaya ya Rorya mkoa wa Mara. Mzee John Obure yeye ni mzaliwa wa Shirati, na alioa mrembo toka kijiji cha Kowak wote ni wana Rorya kwa asilimia 100%!

Mr and Mrs John Obure wakiteta!

Kama wanavyo onekana pichani ni marehemu akiwa na mkewe wakiteta jambo fulani wakati wa msiba wa baba yangu mkubwa mzee Joseph Musira (soma ?) Tanzia: Pumzika kwa amani baba yetu mzee Joseph Musira ….. Marehemu Mzee Joseph Musira alioa first born (mtoto wa kwanza) na Marehemu mzee John Obure alioa second born (mtoto wa pili).

Mama zangu wakubwa mtoto wa kwanza na wapili katika pozi nyumbani kwa Mr and Mrs Musira. Wote ni wakazi wa kudumu hapo Musoma, hivyo ni majirani.

Mama zangu, mabinti wa mzee Cornel Awiti na Valeria Awiti

Pichani ni mama zangu wote 6 kwa ujumla wao. Mwenye nguo ya Orange (rangi ya chungwa) ndio mke wa marehemu mzee John Obure. Bibi yangu mzaa mama alizaa watoto 12 ambao walikuwa mpaka utuuzima! Sita (6 ) wakiume na sita (6) wakike. Wakike wote wapo hai, twamshukuru Mungu kwa hilo. Lakini wakiume wamebaki watatu (3) na watatu wengine wamesha lala usingizi wa mauti. Lakini kiuhalisia bibi yangu alizaa watoto 14! Uzao mmoja ulikuwa pacha (twins) wao walikufa siku waliozaliwa. Twamshukuru Mungu kwa yote.

Pichani juu nikiwa na mama yangu mzazi pamoja na mmoja wa watoto wa marehemu ajulikanaye kama Dr. Joseph John Obure. Hapo ilikuwa ni 2018 Washington DC. Kaka yangu huyu yeye anaishi North Carolina na familia yake.

R.I.E.P baba mkubwa!

Kwa mara nyingine tunatoa pole zetu za dhati kabisa kwa familia ya marehemu mzee John Obure.

“Kwa jasho lako utajipatia chakula mpaka utakaporudi udongoni ulimotwaliwa; maana wewe ni mavumbi, na mavumbini utarudi.” *** Mwanzo 3.19

Bwana alitoa na Bwana ametwaa jina lake lihimidiwe milele zote. ????

Siku ya mazishi

Mke wa marehemu

Dada wa marehemu!
Dada mkubwa wa marehemu

Wajukuu!

mtoto wa marehemu (watatu kuzaliwa) Dr Joseph Obure
Mtoto wa marehemu (wapili kuzaliwa) Deus Obure

Happy birthday Nyasungu!

Happy birthday to the sweetest babysister in the entire world! Thank you for unconditional love and respect you have shown to me that guides me to navigate the joys, the challenges, and understand the responsibilities of being a big sister! Wishing you an extra special day and amazing year! Happy birthday beautiful, love you so very much! ?❤❤❤

Birthday girl herself!
Akiwa na waridi wa moyo wake!
Warombo utawaajua tu!
akiwa na dada yake!
Akiingia kwa birthday dinner yake!

Cake toka kwa wazazi!

Once again, Happy birthday Nyasungu! My mama’s last born, my grandmother namesake, the peace maker, and the charm of our family ?? We love you baby girl! ?❤

Simulizi ya maisha ya mzee O.O Igogo: Baada ya miaka zaidi ya 40 akutana tena na rafiki yake!

“Wilson Simon Mande, aliyekaa kati, leo kampigia simu Mzee OOI na kumjuza kwamba yupo jijini Dar, kitongoji cha Mgeni nani?? Kwa furaha na bashasha nimemuomba niende kukutana naye na ikiwezekana nimkaribishe chakula cha jioni kwetu Kibada.

Mzee Wilson, kaka yangu, rafiki wa kweli na Mfadhili aliyenipa ajira ya kudumu kwenye kampuni ya Kibo Paper Industries Ltd mwaka wa1975, akiwa Afisa Utumishi, nami nikiwa mchoovu asiye na ajira, na aliyekimbiwa na ndugu waliohamia kusikojulikana huko nyuma. Kwa mtonyo wa rafiki yangu Saidi Kikungo a.k.a mapersonality leo hii tumeonana tangia mwaka wa 1978 tulipoachana akiwa Kibo nami nikienda NECO LTD.

Namshukuru Mungu wetu kwa kuniwezesha walau nami nimuonyeshe furaha ya kumbukizi ya wema aliyonitendea miaka hiyo.” 》》》》 Hayo ni maneno yake mzee O.O Igogo mwenyewe siku ya leo 01 /13 / 2021.

WEMA HAUOZI

Vijana wa zamani, waliohitimu elimu ya msingi mwaka 1968 pamoja, wakutana huko Mbande. Mzee. John Wao Abila ( Kati) akipeana mkono na Mzee 0.O Igogo alipomtembelea nyumbani kwa mwanae jioni ya leo.

Historia ya maisha yao Mzee O.O Igogo, alipoteza ajira mnamo mwaka wa 1973, naye akalazimika kujikimu kwa kaka yake mmoja, huku akiendelea kusaka ajira. Baada ya miezi kadhaa siku moja alipotoka mahangaikoni Kunduchi ambapo siku hiyo hakufanikiwa kupata kibarua cha kusaidia mafundi ujenzi, ikambidi kutembea kwa miguu toka huko Kunduchi Beach, hadi Keko Machungwa kwenye maskani ya familia ya kaka yake. Kwa mshangao na butwaa kubwa, alikuta maskani ya kaka yapo holaa! Yaani familia hiyo wamehama nyumba na kwenda kusikojulikana bila ya kumwambia dogo O.O Igogo. Ilikuwa majira inayokaribia saa mbili usiku, hivyo dogo O.O Igogo aliyekimbiwa, naye hana hata senti moja ya kujikimu usiku huo wala kesho yake alijikuta akiangua kilio cha simanzi huku majirani walioambiwa kisa cha kutorokwa wakimcheka kwa kejeli.

Dogo O.O Igogo hakuwa na la kufanya zaidi ya kujiendea kwenye geto lake na kujibwaga kitandani na njaa yake ya kutwa na uchovu wa kutembea zaidi ya kilomita arobaini kwa mguu.

Kati kati ya usiku huo, alisikia hodi mlangoni kwake akiitwa jina na huyo rafikiye John Wao Abila, akamfungulia mlango. Rafiki yake kwa huruma akamweleza sikitiko lake kuhusu hao ndugu waliomkimbia. Hivyo alikuja kumuaomba waende naye nyumbani kwake kupata msosi. Dogo O.O Igogo hakusita, naye wakaongozana kwenda huko kwake. Tangia siku hiyo alikuwa mfadhili wake hadi alipopata ajira kwenye kiwanda cha Kibo Paper Industries Ltd. Rafiki yake alimpa funguo za mlango wake na kumruhusu kujipikia mchana na jioni iwapo yeye atakuwa yupo kazini.

Jana usiku nilimpigia simu ili nimjulie hali huko Utegi, naye akanijuza kwamba yupo hapa Dar. Hivyo ilinibidi kufunga safari na kumtafuta alipo huko Mbande ili nimjulie hali na kusaidiana panapo bidi. Wema wake na fadhali aliyonitendea ni hazina ya milele kwake, namshukuru siku zote, na iwapo pana mahala ana jambo la kumsaidia, siwezi kusita. NIMEFARIJIKA SANA KUMUONA LEO

*** Imeandikwa na Mzee 0.O Igogo November 26, 2020, nimeambatanisha na hiyo ya leo hapo juu kwasababu hii ya November26, 2020 nilikuwa sijaipost humu***

Kheri ya mwaka mpya 2021!

Wapendwa wasomaji wangu natumaini nyote mmekuwa na mwaka mpya mwema, nami naomba niwasalimu kwa kuwatakia kheri ya mwaka 2021. Twamshukuru Mungu tumeuona, naomba ukawr mwaka wa baraka nyingi na amani tele kwetu sote. Mungu atunusuru na pepo la maradhi, vifo, na mahangaiko yasio isha. Kweri na baraka za mwaka mpya.

Nimefungua huu mwaka kwa kuanza kuwarushia picha za wanafamilia ya mzee O.O Igogo walipokutana nyumbani kwa familia ya Nyagilo kwa kusudi la kushiriki chakula cha mchana pamoja maalumu kwa kufungua mwaka mpya ambao tumeanza. ….. Kama utakuwa hufahamu familia ya Nyagilo basi bonyeza ?? Meet the Obama’s extended family members!

Haya mbarikiwe wote!

Pumzika kwa amani ya Bwana mtoto wa dada yangu!

Kutoka kushoto: Alpha mkubwa, Alpha mdogo (R.I.P) na dada Pendo Igogo (mama Alpha).

Pumzika kwa amani ya Bwana wajina wangu Alpha! Ilikuwa heshima kubwa sana pale ulipo zaliwa, dada yangu Pendo Igogo akasema huyu mwanangu nampa jina Alpha kumuenzi mdogo wangu anipendaye sana. Ilikuwa ndio njia pekee ya yeye kunionyesha upendo wake kwangu na jinsi anavyo shukuru kwa upendo wetu kama madada.

Kutoka kushoto: Janeth Igogo, Alpha mkubwa, dada Pendo, Alpha mdogo, na nyuma ni mama yake Pendo mke wa marehemu baba yangu mkubwa.

Alpha, kifo kimeumbiwa mwanadamu lakini sikutegemea maisha yako yangekuwa mafupi namna hii! Leo hii umemuacha dada yangu akiwa si tu mlemavu wa viungo bali moyo uliyojaa maumivu makali sana. The only child she had! Ulizaliwa kama miujiza kwani wengi hata madaktari hawakuweza kuwamini mwanamke mwenye ulemavu wa viungo aina ya mama yako angeweza kubeba mimba kwa miezi tisa na kujifungua mtoto! Na sasa umemuacha mama mkiwa!

Kutoka kushoto: Magreth Igogo, Alpha mkubwa, dada Pendo, Alpha mdogo, na nyuma ni mama yake Pendo mke wa marehemu baba yangu mkubwa.

Baba yako ndie mwanaume aliyempenda dada yangu na akamuoa na Mungu akaibariki familia yao kwa kuwapa mtoto Alpha. Leo hii wote wewe na baba hamponae tena mmemuacha kama alivyo! Kweli maisha ni fumbo na Mungu mwenyewe ndio mwenye kuweza kulifumbua! Nasikiaga wakisema kuwa “ng’ombe wa masikini hazai” na leo umenifanya niamini huu msemo kwa viwango vingine kabisa!

Pumzika kwa amani mrembo, tutakutana asubuhi njema!

Bwana ametoa na Bwana ametwaa jina lake litukuzwe milele! ????