KATAZO LA KUSAFIRISHA MCHANGA WA DHAHABU-2 -Peter Sarungi

KATAZO LA KUSAFIRISHA MCHANGA WA DHAHABU 2

Peter Sarungi (The next time)

Sehemu ya II – Ijue Sector ya Madini Tz

Sector ya madili ilianza kutambulika rasmi wakati wa utawala wa awamu ya tatu chini ya Raisi mstaafu Mh. Ben Mkapa kupitia sera ya uwekezaji. Mh. Mkapa aliamini maendeleo ya nchi yatasaidiwa ikiwa tuta ruhusu uwekezaji mbalimbali ikiwemo sector ya madili. Aliamini nchi itafaidika kwa kupata teknolojia mpya, mitaji mikubwa, elimu mpya katika sector hiyo pamoja na kuongeza ajira kwa wananchi na mapato ya serikali. Wawekezaji wakubwa walianza kujitokeza mwaka 2001 Geita na Kahama. Madini yanayopatikana nchi ni mengi kwa aina tofauti kama vile dhahabu, almasi, ruby, Tanzanite, Copper, Silver na mengine mengi ingawa zaidi ya 80% ya machimbo nchini yanajihusisha na uchimbaji wa madini ya Dhahabu. 

UZALISHAJI WA DHAHABU

Mpaka sasa tuna machimbo makubwa ya dhahabu yapatayo sita ambayo ni Bulyanhulu(BGM), Geita(GGM), Buzwagi(BZGM), Biharamulo, North Mara na New Luika. Kwa mwaka migodi hii huzalisha 1.37Million troy ounce ambayo ni zaidi ya kilogram 50,600 ya dhahabu safi kwa mwaka huku GGM ikiongoza kwa uzalishaji wa 38.6% na ya mwisho ikizalisha 1.5%. Kwa viwango hivi, Dhahabu inachangia zaidi ya 90% ya uzalishaji wa madini yote inchini kwa mwaka.

               NJIA ZA UZALISHAJI

Uzalishaji wa dhahabu upo wa aina mbili maarufu ingawa kuna nyingine ya tatu, aina hizi zinatokana na utofauti wa miamba ambayo dhahabu hupatikana. Kuna miamba ambayo ina oxide na zingine zina sulphide.

Dhahabu inayopatikana katika Miamba yenye oxide ina zalishwa kupitia njia za gravity na Cabon process (cabon in loucher CIL na cabon in pulmp CIP). Njia hizi ni common na zipo nyingi katika migodi yetu hadi kwa wachimbaji wa kati. Migodi yenye miamba ya oxide inayotumia njia hii ni nne kati ya zile sita yaani GGM, North Mara, Biharamulo na New Luika. Hivyo uzalishaji katika migodi hii hufanyika na kumalizika ndani ya nchi. Migodi hii haisafirishi mchanga kwenda nje.

Dhahabu inayopatikana katika miamba yenye sulphide ina zalishwa kupitia njia ya gravity, caborn process na kuhitimishwa na smelter. Njia za gravity na Carbon process huzaliza 40% pekee huku smelter ikizalisha 60% ya dhahabu. Dhahabu inayopatikana katika miamba yenye sulphide ina ugumu wa kunyonywa kupitia njia zilizopo nchini kutokana na dhahabu hiyo kuungana na madini mengine ya copper na silver, hivyo ili kuitoa dhahabu hiyo ni lazima uwe na tanuru kubwa (smelter) lenye uwezo wa kuyetenganisha madini hayo kutokana na utofauti wa melting point za madini hayo. Hivyo ni lazima mchanga unaozalishwa baada ya mchujo kwa njia za kwanza usafirishwe kwenda nje kwaajili ya kuzalisha 60% iliyobaki. Migodi yenye miamba yenye sulphide inayotumia njia hizi zipo 2 kati ya sita nazo ni BGM na BZGM. Migodi hii ndioyo husafirisha mchanga kwenda china na japan 🇯🇵 kwaajili ya uchenjuaji.

Mpaka hapo kama kuna swali unaweza kuuliza kabla sijakwenda mbele zaidi. Uliza ndani ya maelezo hayo, usitoke nje maana bado kuna makala nyingi zinakuja

Asanteni.

KATAZO LA KUSAFIRISHA MCHANGA WA DHAHABU -Peter Sarungi

KATAZO LA KUSAFIRISHA MCHANGA WA DHAHABU

Peter Sarungi (The next time)

Sehemu ya I – Utangulizi

Mkuu wa Kaya ali ahidi kusimamia sector ya madini kwa umakini ili sector hiyo iweze kuleta tija na faida kwa Taifa. Hivyo serikali ya Mkuu wa kaya imezuia usafirijashi wa mchanga wa dhahabu kwa makampuni ya uchimbaji yaliyopo nchini kwa muda usio julikana.

Lengo la zuio hilo lililotokana na kauli za mkuu wa kaya ni kuhakikisha serikali ina ondoa mianya ya kuibiwa madini hayo ambayo yana chujwa nje ya nchi huku sisi tukipewa mrejesho ambao kwa hisia za mkuu wa kaya anao mrejesho bado una ukakasi. Lakini pia mkuu wa kaya alitamani kabla ya kuwa Mkuu na anaendelea kutamani kujengwa kwa hilo Tanuru kubwa la kuchuja dhahabu, shaba na copper hapa Tanzania ili kufikia ndoto za kuwa na Tanzania ya Viwanda.

Pamoja na dhamira njema ya mkuu wa kaya, ni vizuri na sisi watanzania tukajua kinachoendelea katika sector hii ili tupate kujua faida na hasara za zuio hili ikiwa ni pamoja na changamoto za kufikia shauku la mkuu wa kaya la kuwa na Tanuru hilo lijulikanalo kama Copper Concetrate Smelter  Hivyo nita toa makala ya kueleza hali halisi za sector hii ikiwa ni sehemu ya kwanza na makala nyingine ya kueleza faida, hasara na changamoto ya kufikia ndoto ya mkuu wa kaya ya kuwa na Tanuru la kuchuja madini hayo Tanzania.

Nitatumia vikao mbalimbali nilivyoweza kuudhuria vya wataalum wa madini, ripoti mbalimbali kutoka TMAA na machapisho mbalimbali ya kimataifa kama vyanzo vya habari katika kusapoti andiko langu.

Asanteni

“Republicans and their “pipe dream” of appealing and replacing Obamacare.” – Chege Kilahala

Republicans and their “pipe dream” of appealing and replacing Obamacare…….

If you can’t marshal enough votes in a house (the congress) where you have a comfortable majority. Then your chance of passing it the senate where you have a very thin majority is non-existent…..

Now, we can toast and celebrate that, Obamacare is the law of the land….and it will carry on being so…….I look forward to seeing a universal healthcare system in the USA; one day soon. Just like whats found in Canada and Scandinavian countries….

UKIMWINDA SANA MJUSI ANAGEUKA NYOKA. -Peter Sarungi

UKIMWINDA SANA MJUSI ANAGEUKA NYOKA. 

Peter Sarungi (The next time)

Huu ni msemo wa wahenga ambao uhalisia wake unaonekana mara chache porini lakini hutokea sana kwa maisha ya binadamu. Naamini kuna watu walisha wahi kumwinda mjusi kipindi walipokuwa watoto na katika kumwinda mjusi gafla walipo toa jiwe wakakutana na nyoka, inapofika hapo lazima hali ya hatari itatokea.

Naiona nchi yangu kwa mbali inakaribisha hali ya hatari. Mkuu wa kaya alianza kuongoza nchi yake kwa misingi ya sheria huku akijitambulisha kuwa yeyeni mkali kwa maneno na matendo yake. Baada ya kuwa mkali sana watoto wakaanza kulalamika huku wakionesha kuto ridhika na maamuzi ya baba. Watoto wakaanza kumwinda baba kwa vifungu vya sheria huku wakimtangaza baba kuwa ni dikteta. Na kwa jinsi baba alivyo na msimamo, hakuwahi kurekebisha makosa yake hasa yale yaliyovunja sheria na hata kuonesha upendeleo wa wazi wazi huku akiwagawa watoto wake kwa kauli na matendo.

Kwa sasa hali imekuwa mbaya maana watoto wameanza kumkana baba yao kwa kutumia mama yao Katiba. Wana mshawishi mama yao (Katiba) awaoneshe baba mwingine kwa kutamka kuwa huyu sio baba mzazi na wamtafute baba mwingine.

Kwa hatua ya mawindo yalipo fikia,  nawaona watoto wanahisi wanaye  mwinda ana fanana na Mjusi hivyo wanaongeza jitiada za makusudi wakiamini nguvu za mjisi zipo mkiani na wala sio nguvu za kuogopesha kiasi cha kutaka kumtoa kwenye pango lake.

Lakini nahofia sana hasira za baba, baba akikasirika na kuamua kutumia nguvu zake basi anaweza akawalazimisha watoto kuendelea kuitwa baba kwa kumtishia mama na hata kuwa adhibu vikali watoto wanao kwenda naye kinyume, na akiona bado anapingwa basi anaweza kumbadili mama mwingine na kufunga ndoa ya kudumu. Kwa hatua hii, baba hatakuwa tena mjusi bali atakuwa ni nyoka.

Kwa sasa watoto wajiandae kukutana na nyoka katika mawindo yao, wasidhani wataendelea kukutana na mjusi walie mzoea kumwinda. Wajiandae na plan B,C na hata C ya kukutana na Nyoka.

By the way baba amesha geuza kichwa bado mkia wa nyoka tu aanze mashambulizi kwa watoto wanao winda. 

“Be careful and watch it” Mkuu wa kaya 24/3/2017

“Did Magufuri’s decision to appoint him as the RC base on the qualification he claimed to have?!!!” -Chege Kilahala

If I apply for a job that requires a qualification A and I get offered the job on the basis of my qualification A, then if my employer finds out that, I didn’t possess that qualification, he/she will have the “legal basis” to terminate my employment on that fact……….But if I apply for a job that does not specify that it requires any qualification, but I falsely put down that I possess qualification A, my employer WOULD NOT HAVE any legal basis to terminate my employment on that fact. It is because, his decision to employ me was not influenced by the fact that I have  or have not had that particular qualification.

For that reason, why do people ask for the resignation of Paul Makonda from the RC position? Did Magufuri’s decision to appoint him as the RC base on the qualification he claimed to have?!!! Do you need to even have a standard 7 qualification to be appointed as an RC??!! Leave the guy alone………….!!!

“Sikiliza Zitto Kabwe” Jerry C. Muro

Sikiliza Zitto Kabwe

Mungu amewapa wenzetu “wazungu” baraka ya utajiri wa technology.

Na pia ametupa sisi watanzania baraka ya utajiri wa Udongo wenye thamani.

Ili technology yao ifanye kazi inahitaji malighafi kutoka kwetu.

Sio busara na hekima kuwapelekea malighafi wao mana haiwezi kuhamishwa, ILA TECHNOLOGY INAHAMISHWA.

WAJE WALETE TECHNOLOGY TUTAZUNGUMZA NAO. Jerry C. Muro

Machame, Hai

Kilimanjaro.

26/03/2017

KAMA NAPE KAFANYIWA HAYA, VIPI KWA MTI MKAVU?. -Peter Sarungi

Peter Sarungi (The next time) Injili ya yesu ilipata kumnukuu Nabii Issa (Yesu Kristu) alipokuwa njiani kusulubiwa baada ya kukutana na wamama wakimlilia kwa uchungu,  sehemu ya nukuu inasema ” ikiwa wanafanya haya kwa mti mbichi, je itakuwaje kwa mti mkavu???? 

Kwa kawaida mti mbichi una sifa za kuvumilia shida, ni mgumu kuvunjika lakini vilevile ni mti unao onesha uhai, wenye kuwa na afya ya kustawi na ni mti unao weza kuzaa matunda tofauti na sifa za mti mkavu ambao kwa ujumla unatambulika kama mti ulio kufa.

Namfananisha Mh. Nape Nnauye na mti mbichi ndani ya CCM. Kila mtu anajua mti huu mbichi ulivyo kuwa na uhai, wenye afya na aliyeweza kuitetea chama hadi kupata matunda ya kushika hatamu. Nape amesema alilala porini siku 28 kwaajili ya kuhakikisha chama inapata ushindi, amekipigania chama hadi kufikia kutoa utu wake kwa kukubali lawa, dhiaka na chuki kutokana vita ya kutetea chama kipindi kigumu cha uchaguzi 2015. Inawezekana ile kauli ya Bao la Mkono aliyosema Nape ndio aliyokuwa akitumikia porini kwa siku 28.

Lakini leo, Mti huu hauna tena dhamani mbele ya bashite, mti unatendewa yale wanao tendewa wapinzani wa leo. 

Ikiwa haya yametendwa kwa mti mbichi kama Nape, Je ni nani aliye salama hasa kutoka mti mkavu kama mimi?????

Pole Nape, najua sasa zile akili za kushikiwa na chama utakuwa ume waachia wengine ambao bado wana imani ya kuchukua nafasi yako.

By the way wewe unaye jiita mwana CCM na mkereketwa wa zidumu fikra za mwenyekiti, anza kujiandaa kisaikolojia ili usije pata strock kwa maamuzi kama haya. Chama kwa sasa kina mwenyewe….

Baba yangu Dr. Magufuli mbona unatuangusha hivyo?!!- Alpha Igogo

Baba naomba nianze kwa salamu; shikamoo baba!…….Baba naomba nikwambie dhumuni la barua hii si kukuomba hela za matumizi kwani hilo si tatizo langu kwa sasa! Pesa zipo tena wewe wenyewe ndio umeziweka hivyo nipo vizuri baba!

Alpha Igogo, Blogger

Baba ninachotaka kukwambia leo hii nakuomba utege masikio yako kwa makini sana baba yangu kwani mwanao nimejawa na hofu nyini sana! Wewe ni baba yangu ninaye kupenda sana na siku zote nilitembea bara-barani na kulala usingizi mnono sana nikijua tupo katika mikono salama! Lakini, sasa hivi uwoga umenishika sana, siyo tu kwa watu ambao siwajui bali hata kwa hawa wakuu wa mikoa yetu ulio wachagua. Na mbaya zaidi imani yangu juu yako imeshuka kwa kiasi kikubwa sana kitu ambacho si kizuri kabisa kwani wewe ni baba yangu!

Baba, naomba unisaidie kuelewa, kwani unampango wa kung’ang’ania madarakani? Au unataka nchi yetu iwe kama Rwanda ile ya mauwaji?  Au kama Uganda ya Mseven? Au unatamani Tanzania iwe kama Congo ya Kabila, na Burundi ya Nkurunzinza?! Au iwe nchi ya ukabila kama ile nchi ya Jomo Kenyatta?!! Mimi sijui baba lakini natamani kujua, tafadhali nijuze ili nijuwe kama nianze kuomba ukimbizi nchi za jirani?! Nakama ni hivyo je, zitakua ni nchi zipi katika bara hili la Africa?!!

Baba, niwapi mimi binti yako nikimbilie maana dalili zinaonyesha kama hali itaendelea kuwa hivi na wewe ukaendelea kubariki kwa mikono yako miwili basi mimi mwanao sina budi kuanza kukimbia kuomba hifadhi nchi za jirani hata ng’ambo ya Magharibi kama itaibidi! Japo natafakari sana je nitakimbia mwenyewe au nimchukuwe na mama? Vipi kuhusu bibi na babu? Bila kumsahau mjukuu wako kipenzi! ooh! vipi na yule dada yako wa pekee aliye olewa kijiji cha Koromije mkoani Mwanza? tena yeye ni mlemavu wa miguu! Na binamu yako Zainabu ambaye ni mlemavu wa ngozi huwa awezi tembea juani! Hawa wote nawapenda sana na itakuwa ngumu sana kwangu mimi kuishi mbali nao, nifanyeje baba? Hivi mida ipi itakuwa mizuri kwetu sisi kuanza mwendo; mchana au usiku? Baba, nguvu zinaniishia! Baba kwani niwapi tulikosea? Mbona mambo yanakuwa tofauti na ahadi zako? Mimi niliwashawishi ndugu zetu wote, majirani, marafiki, na Watanzania wote kwa ujumla kuwa wakupigie kura ya “ndio” kwani nina imani nawe, na kwa uchapa kazi wako ulionyesha kuwa wewe unafaa sana! Nao kwa furaha na nderemo wakakupitisha kwa kishindo kuwa Rais wa nchi yao. Nami mwanao nikatembea kifua mbele tena kwa mikogo na madaha mengi sana kuwa sasa Tanzania mpya inakuja! Tanzania ya amani tele, iliyo jaa demokrasia nyingi na uhuru wa kujieleza bila vitisho! Tanzania ya viwanda na miundo mbinu ya kisasa!

Baba, sasa mbona mambo yanakwenda sivyo?! Uliahidi kuleta uongozi bora ulio tukuka, uongozi wa haki na wakufuata sheria. Uliahidi kutulinda sisi wanawake na watoto, ukatuhakikishia kuidumisha amani ndani ya nchi yetu tuipendayo sana! Imekuaje sasa? mbona wavunja sheria ndio unawatukuza na kuwatunuku shahada za uongozi bora?! Baba ni wapi tumekukwaza? Mbona viongozi wanao tishia usalama wa maisha yetu kwa kuvamia sehemu zetu za kazi kwa mitutu ya bunduki ndio unao wapenda sana? Usalama wetu upo wapi? Mbona ndugu zangu hata hawaruhusiwi kuongea kwa uhuru bila kutolewa silaha za moto?!

Baba, nampenda sana kaka yangu ambaye ulimchagua kuwa mkuu wa mkoa wa Dar es salaam. Nimchapa kazi sana hilo halina upinzani lakini baba yeye si mkamilifu, ana mapungufu yake kama mwanadamu yoyote yule; hivyo kubali kuwa sanyingine naye hukosea. Basi anastahili kuadhibiwa kama unavyo tuadhibu sisi wanao wengine kwa makosa tunayo yafanya au pale tunapo kukwaza!

Baba, sababu ya mimi na Watanzania wengine kuomba umuadhibu huyu kaka yetu, si mbaya hata kidogo! Hatuna nia ya kumkomoa au kumuumiza bali nikutaka kuweka mfano mzuri kwa wadogo zetu ambao wanakutizama iliwajifunze kitu fulani kuhusu utawala bora wa sheria na haki. Maamuzi yako  yatatuaminisha kuwa unamaanisha kile usemacho. Kufanya hivyo kutaondoa hofu tulionayo Watanzania. Au unaogoapa hutopata mchapa kazi kama yeye? mbona kule kanda ya ziwa wapo wachapakazi wengi sana, tena watiifu, na waaminifu, hawana uonevu wala kiburi?!

Baba, naomba nimalizie kwa kusema samahani sana kama tumekukosea. Lakini ukumbuke tu kuwa wewe ni baba wa wengi na si wa mtu mmoja tu, hivyo tunaomba utupende, na utulinde wote bila ubaguzi wa aina yoyote! Usitugawe baba sisi sote ni wana wako. Sisi ni ndugu moja japo wengine ni wembamba na wengine wanene. Japo wengine wafupi na wengine warefu, wengine weusi wa rangi ya ngozi na wengi ni maji ya kunde; sisi ni ndugu moja. Usitubague wala kututenga!

Asante sana baba.

KUNA GHARAMA KUTETEA UKWELI – NAPE!

KUNA GHARAMA KUTETEA UKWELI – NAPE

Peter Sarungi (The next time)

Nimesikitishwa sana na taarifa kutoka ikulu, ingawa niliona ishara hiyo kutokana na mwenendo uliopo. Pamoja na hayo Nampongeza sana Mh. Nape Nnauye kwa karata ya ushindi aliyo cheza jana kwa maamuzi ya kutetea ukweli. Kwa karati hii, watanzania wamefuta Hasira, dhiaka na chuki walizokuwa nazo toka kipindi ulipo kuwa Msemaji wa propaganda za chama. Leo Umekuwa shujaa wa uhuru wa habari na naamini hivi vyombo vya habari vitakutunuku kwa maneno na matendo kwa kutetea ukweli. Nakutakia safari njema ya siasa, ukiweza basi anzisheni chama chenu wanasiasa wote mnao tengwa na chama kwa kuwa tofauti na mkuu maana sioni chama mbadala kitakocho wapa uhuru wa kufanya siasa zenu.

“TLS ; CHADEMA’s legal department or another opposition party?!!!” – Chege Kilahala

TLS ; CHADEMA’s legal department or another opposition party?!!! There are legal boundaries within which these institutions can carry out their daily duties……using TLS as a mouthpiece to pursue some political agenda is a no-no-no-no!!!  

Happy birthday Hoyce Temu!

Mmoja wa Malkia wetu wa nguvu leo kazaliwa! Kheri na furaha ya siku ya kuzaliwa dada Hoyce temu! Asante sana kwa kuwa nguzo imara na mfano mwema wa kuigwa kwa wanawake wa taifa la Tanzania. Asante sana kwakuonyesha njia watoto wetu na wadogo zetu.

Katika siku hii kuu ya kuzaliwa kwako tunakuombea afya njema, amani, furaha, na upendo mwingi! Mungu azidi kukubariki sana dada Hoyce! Happy birthday to you! 💜💜💜

I upgraded Ruge Mutahaba!

Mmeona shemeji yangu Ruge jinsi alivyo ongea kisomi?! ‘Kijana’ kaongea kwa ma-confidence kama Rais bwana  (in Haya’s accent)! Yani huyu Muhaya ni kichwa usipime! Na sasa nimeamua kum- upgrade siyo Loser tena ni Hero wa Watanzania. Na kwakuwa ni mambo ya kupokezana kijiti basi kijiti chake kipo pending kwasasa mpaka report ile ya tume ya Nape Mnauye itakapo kamilika halafu tutamkabidhi mtu fulani 🙁  …… Huko nyuma nilisemaga hivi TheTwoBiggestLosers  🙂 🙂 kwakweli nimecheka sana! What was I thinking?! Kha! Ogopa mwanamke akiwa amekasirika 🙂 🙂

Halafu mimi sipendi tabia ya watu wanao bugudhi Wahaya!! Mnajua mie nina ubiya wa kudumu na Wahaya 🙂 🙂  leave my Hayas’ alone peeople!!  …… Haya Ruge nitafute uchukue hela yako ya lunch umefanya kazi nzito sana 😉 😉

UKIPINGWA NA MKUU, VIZURI UKAJIWAJIBISHA. -Peter Sarungi

UKIPINGWA NA MKUU, VIZURI UKAJIWAJIBISHA!

Peter Sarungi (The next Speaker)

Ingawa ni vigumu kupata tamaduni za kuwajibika kwa viongozi wengi wa Afrika lakini bado kuna kila ulazima wa kuwakumbusha viongozi wetu na hata kuwafunza vijana ambao ni kizazi kinachochukua dhamana kutoka kwa wazee wetu juu ya umuhimu na faida za kuwajibika mwenyewe bila kushurutishwa.

Watanzania tunafunzwa na viongozi wetu kuwa na tabia za ajabu sana unapopata madaraka, tabia kama za ubabe, majivuno, dharau, ung’ang’anizi, ufisadi, uzembe na zingine nyingi ambazo tumekuwa tukizishuhudia kutoka kwa viongozi wetu. Tamko alilotoa Waziri wa Sheria la kupiga STOP ufungaji wa ndoa bila cheti cha kuzaliwa kuanzia mwezi wa tano na baada ya muda mfupi Mkuu wa kaya akatoa katazo la utekelezaji wa agilo la waziri wake. 

Kwa tafakuri ndogo, inaonesha kwamba agizo hilo la waziri halikupata utafiti wa kutosha na pia halukupita kwenye vyombo vya ushauri kama Baraza la mawaziri. Pia inaonekana agizo hilo limemkera sana Mkuu wa kaya kiasi kwamba akalitolea tamko yeye mwenyewe bila kutumia wasaidizi wake kama vile waziri aliye husika kutoa agizo hilo.

Kwa maamuzi aliyoyafanya Mkuu wa nchi kwa Waziri husika lina fundisho kubwa sana na angalizo kwa waziri husika. Ningekuwa mimi ni waziri husika ninge jiwajibisha kwa kushindwa kufikia viwango vya mkuu wangu wa kazi, maana inawezekana akanitumbua ama akanisahau kwenye marekebisho ya baraza la mawaziri.

Nafikiri ni muda mzuri kwa Waziri Mwakiyembe kuji pumzisha ikiwa ni hatua ya kujiwajibisha ili aendelee kubaki na heshima yake iliyo tukuka kwa nchi. Kuna faida kubwa ya kujiwajibisha mwenyewe kuliko kusubiri kuwajibishwa tena kwa aibu, nasema hayo kwa sababu na mimi mpaka leo naendelea kunufaika na hii tabia ya kujiwajibisha ambayo nimewahi kuifanya sehemu mbalimbali za uongozi wangu.

By the way kuna kazi sana kutoa tonge kutoka kwenye midomo ya waafrika, wapo tayari kunyang’anywa kwa nguvu kuliko kulitema wenyewe hata kama tonge ni chungu.

Asanteni.

“Sir George Kahama ni moja ya Tunu za Taifa” -Shy-Rose Bhanji

Mbunge wa bunge la Afrika Mashariki Hon. Shy-Rose Bhanji ametoa salamu zake za kuguswa na kifo cha aliyekuwa mtumishi wa umma  wa muda mrefu Sir George Kahama kwa kusema haya “Sir George Kahama ni moja ya Tunu za Taifa kwa mchango wake ktk Serikali za Mwalimu Nyerere, Mzee Mwinyi na Mkapa…Asante kwa utumishi wako uliotukuka wa kulitumikia Taifa la Tanzania. Mungu akulaze pema Baba 🙏 Pole nyingi kwa Familia yote Mungu awape nguvu na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu #SirGeorgeKahama #RIP” ……. Muheshimiwa Shy-Rose aliyasema hayo mapema leo kupitia kurasa zake za jamii (Facebook, Instagram). Nami naomba kuungana naye kwa niaba ya familia ya mzee O.O Igogo kuwatakia pole wana familia yote, ndugu, marafiki, na jamaa. Poleni sana kwa msiba huu Mungu aendelee kuwa nanyi wakati wote……….Bwana ametoa na Bwana ametwaa jina lake lihimidiwe milele zote!

“NIMECHAGUA UKWELI KWENYE SIASA, SIO BARIDI WALA MOTO.” -Peter Sarungi

Peter Sarungi (The next Speaker)

Siasa safi zinahitaji kuwa na demokrasia ndani yake, kuwe na uhuru wa kutoa mawazo mbadala, kuwe na desturi ya kuvumiliana hasa pale mnapopingana mawazo na kuwe na tabia ya kutafuta na kusema ukweli hata kama ukweli huo utakuwa mchungu.

Mtindo wa vijana wengi wa sasa ni wa ajabu sana katika siasa. Mtindo ulio gubikwa na tabia za uongo, unafiki, fitina, wasaliti, ndumilakuwili, kujipendekeza, kutafuta sifa, kukurupuka, ushabiki, na unazi usiokuwa na tija kwa taifa. Tabia kama hizi zina fifisha ubunifu, uzalendo, umakini, ujasiri na umahiri kwa vijana katika uongozi na uwajibikaji.  Tumejenga jamii ya vijana walio gawanyika kihisia, itikadi, maneno na kwa matendo yao, waoga wa kutetea ukweli, wepesi wa kushindwa na uovu, walio tayari kusema vya kukaririshwa. Ndio maana kuna vijana walio tayari kukosoa jambo lolote kutoka upande wa pili hata kama ni jambo jema kwa taifa na wapo tayari kusifia jambo lolote la upande wao hata kama ni sumu kwa Taifa. Wameamua kuwa baridi ama moto.

Mimi nimekataa kuwa sehemu yao, kuwa mtumwa wa fikra zao, kutumika katika malengo yao. Nimeamua kuwa mfuasi wa ukweli na kwa fikra huru. Nahitaji Ukweli ili uniweke Huru, ukweli utakao tibu Taifa ili vizazi vijavyo vipate kufaidika na ukweli huu.

Unga kuchagua ukweli ili tujenge Taifa lenye kuheshimu ukweli.

Asanteni sana.

Blog